Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Majaliwa: tutaendeleza mashusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) litaendelea kuimarisha mahusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Morocco ili tuweze kunufaika zaidi katika kukuza kiwango cha mpira wa miguu .

Amesema hayo jana (Alhamisi Julai 15, 2021) baada ya kutembelea Ofisi za Shirikisho hilo na eneo la Mchezo wa Mpira wa Miguu la Mohammed wa VI kuona uwekezaji wa miundombinu ya mpira wa miguu uliofanywa katika eneo hilo

Amesema kuwa Shirikisho hilo liendelee kutumia fursa ya mafunzo kwa pande zote mbili lengo likiwa ni kuwa na timu za taifa zilizo bora na zenye ushindani kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Morocco.

Aliongeza kuwa shirikisho hilo limekuwa likiisadia sana Tanzania katika kujifunza mbinu mbalimbali za kiutawala pamoja na mbinu za kimichezo kupitia timu za taifa za Tanzania.

“Timu zetu za taifa za Taifa Stars, Serengeti Boys, Ngorongoro na Twiga Stars zimekuwa zikija hapa Morocco kuweka kambi kwa gharama ya Serikali yao hili ni jambo kubwa na la kuendeleza”

Kadhalika Waziri Mkuu alisema kuwa katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani alikumbushia ahadi ya Mfalme wa nchi hiyo juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Mohammed VI uliopangwa kujengwa jijini Dodoma “tumemkumbusha na ameahidi kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kumkumbusha mfalme ili ujenzi uanze kwa kuwa kila kitu kipo tayari”

-End-