Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi aridhishwa na maandalizi ya kuelekea Kilele cha Mdahalo wa Taifa wa Mausuala ya UKIMWI


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameeleza kuridhishwa na maandalizi ya kuelekea siku ya kilele cha Mdahalo wa Kitaifa juu ya Mwitikio wa UKIMWI Tanzania itakayofanyika tarehe 07 Septemba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa ameridhishwa na hatua ya maandalizi hayo huku akitumia    hilo kueleza mikakati ya Serikali katika kuhakikisha mapambano dhidi ya UKIMWI yanaendelea ili kuyafikia malengo ya sifuri tatu ifikapo 2030.

“Hadi sasa maandalizi yamefikia asilimia 95 hivyo nitoe wito kwa wananchi kufuatilia tukio hili ambalo litarushwa katika vyombo mbalimbali vya habari ili kuendelea kupata uelewa kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI”, Alisema Dkt. Yonazi

Kaulimbiu ya Mdahalo huo ni; “Imarisha ubia na ushiriki wa jamii, kwa mwitikio endelevu wa UKIMWI Tanzania,”

 =MWISHO=