Habari
Dkt. Yonazi aongoza kikao cha 13 cha Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha 13 cha Kamati ya Taifa ya Ushauri ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kilichofanyika tarehe 15 Disemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam (JINCC).