Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Uongozi Taasisi ya ESRF


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja kwenye masuala ya kisera, ikizingatiwa kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni Mratibu wa masuala ya sera za Kitaifa.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 26 Februari, 2025 ofisini kwake Jijini Dodoma.