Habari
Dkt. Biteko aungana na Wanabukombe kwenye mbio fupi
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko leo Oktoba 10, 2024 ameungana na wananchi wa Bukombe kwenye mazoezi ya kukimbia mbio fupi za KM 5 ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani ambayo yanafanyika Wilayani Bukombe, Oktoba 11, 2024.
Katika mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhe. Paskasi Mulagiri, Viongozi mbalimbali wa Wilaya pamoja na benki ya CRDB wameshiriki.