Habari
Dkt. Biteko atembelea vituo vya ITV na Redio One
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Agosti 26, 2024 amefanya ziara katika vituo vya utangazaji vya ITV, Redio One na Capital TV vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika vituo hivyo Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vituo hivyo Bi. Jocye Mhavile kisha akapata fursa ya kutembelea studio mbali mbali na kupewa maelezo kuhusu utendaji kazi wao.