Habari
Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia nchini Namibia
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 2, 2024 amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, nchini Namibia kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Hydrogen Barani Africa (Global African Hydrogen Summit) utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia Septemba 3 hadi 5, 2024.
Dkt. Biteko na ujumbe wake wamepokelewa na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Thobias Lebbius akiambatana na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Caesar Chacha Waitara.