Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko amfariji Angelah Kairuki


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 10, 2024, amesaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa Mzee Peter Orgones Mkwizu, Baba wa Mhe. Angelah Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum na Mshauri wa Rais.

Dkt. Biteko amefika nyumbani kwa Mhe. Kairuki, Tegeta, Jijini Dar es Salaam kufuatia msiba huo uliotokea tarehe 9 Septemba, 2024 katika Hospitali ya Lugalo alipokuwa akipatiwa Matibabu.

=MWISHO=