Logo
Developed by JoomVision.com

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 23, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege kabla ya mazunguzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 23,2015.

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine(SYG)kilichopo mkoani Dodoma Bw.Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw.Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda,Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezi vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.

Waziri Mkuu,Mhe Mizengo Pinda(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.

Makamu wa Rais,Dkt.Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam,nyumbani kwa marehemu,Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu,aliyefariki Septemba 17, 2015.Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wafanyakazi wa Benki kuu ya Tanzania wakati alipotembelea banda la la Benki hiyo baada ya kufungua maonyesho ya Nanenane kwenye uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 4,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akitazama mashine ya kunyonyoa kuku wakati alipotembelea banda la kampuni ya ubia kati ya watanzania na wachina ya Poly Machinery ya Millennium Busibess Park jijijni Dares salaam, baada ya kufungua maonyesho ya Nanenane kwenye uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 4,2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua maonyesho ya Nanenane Kitaifa kwenye uwanja wa Ngongo Lindi Agosti 4,2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa lindi, Mwantumu Mahiza na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwa amekalia moja ya madawati mapya ya plastiki yaliyowekwa kwenye moja ya madasa ya shule ya msingi ya Kakuni wilayani Mlele akiwa katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni Julai 16,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt.Ibrahim Mzengi wakati aliposoma taarifa fupi ya mkoa huo baada ya Waziri Mkuu kuwasili Mpanda mkoani Katavi kwa mapumziko mafupi Julai 15,2015.Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo,Mhandisi Emmanuel Kalobelo.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na viongozi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda Julai 15,2015.Mheshimiwa Pinda atakuwa Mkoani Katavi kwa mapumziko mafupi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri Mkuu wa Ethiopia,Hailemariam Desalegn wakati mgeni huyo alipoondoka nchini baada ya ziara yake ya siku moja Juni 2, 2015

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Wahandisi na Mafundi wa Kichina wanaojenga mtambo wa kuchakata gesi kwa gharama za serikali kupiatia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)katika eneo la Madimba mkoani Mtwara Julai 1,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimsindikiza Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ambaye anapunga mkono wakati mgeni huyo alipoondoka nchini baada ya ziara yake ya siku moja Juni 2, 2015.

Waziri mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na fundi cherehani Abdallah Nyangalilo ambaye ni mlemavu asiyoona wakati alipotembelea bada la mlemavu huyo katika maoyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 3,2015

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watu waliofika kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumsikiliza wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015.

Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi waliofika kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma kushuhudia wakati Waziri Mkuu,Mizengo Pinda alipochukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12,2015.

Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua kundi la waamuzi na walimu wa michezo wa shule za sekondari baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akipiga mpira wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Juni 10,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Nyamagana,Ezekia Wenje,Bungeni mjini Dodoma Juni 11,2015.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima(kulia)Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai,Freeman Mbowe (wapili Kulia),Mbunge wa Viti Maalum,Rose Kamili (wapili kulia)na Mbunge wa Viti Maalum Susan Kiwanga(kushoto)kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 11,2015.

Other News and Events

Ofisi ya Waziri mkuu yaibuka mshindi wa kwanza Nanenane

Ofisi ya Waziri mkuu imeibuka mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za jamii zilizoshiriki katika m...

Read more

Serikali za vijiji zatakiwa kuhusisha Maafa ya mabadiliko ya tabianchi na mipang

Serikali za vijiji zatakiwa kuhusisha Maafa ya mabadiliko ya tabianchi na mipango ya maendeleo. Of...

Read more

News in picture

Developed by JoomVision.com

Mjumbe wa Kamati ya Maafa wilayani Mpwampwa, Shekh,Sabah Seif akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino,Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,tar 12Septemba,2015.

Mkuu wa Mkoa Dodoma, Luteni.Mstaafu,Chiku Galawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,tar 12Septemba,2015.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro,Noel Kazimoto akikabidhi mpango wa Kujiandaa na kukabili maafa wilayani Mvomero kwa Katibu Tawala wilaya ya Mvomero,Veronica Kinyemi wakati wa Uzinduzi wa mpango huo leo tar 3Septemba,2015, anayeshuhudia ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brig.Gen,Mbazi Msuya.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Gen,Mbazi Msuya akisisitiza umuhimu wa Mpango wa Kujiandaa na kukabili maafa kwa wilaya ya Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro wakati wa Uzinduzi wa mpango huo leo tar 3Septemba, 2015.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt.Florens Turuka akiagana na mwenyekiti Kijiji cha Mwakata Kahama,Ezekieli Ramadhani baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa mvua zilizojengwa na SUMA JKT,tar 30 Agosti,2015,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT na Kanali Felix Samillan na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brig.Gen,Mbazi Msuya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt.Florens Turuka(mwenye miwani)akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Patrick Karangwa wakati alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa Kijijini Mwakata,Kahama,tar 30 Agosti, 2015.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brig.Jen Mbazi Msuya akieleza jambo wakati wa Warsha ya Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali leo,tar 20Agosti,2015,Jijini Dar es Salaam.

Mtaalam wa Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka UNDP,Abbas Kitogo akieleza jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali leo,tar 20 Agosti,2015,Jijini Dar es salaam,kushoto kwake ni Mratibu wa mradi huo,Ofisi ya Waziri Mkuu,Bw. Alfei Daniel.

Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brig.Jen Mbazi Msuya(wapili kushoto waliokaa),baada ya ufunguzi wa warsha hiyo leo,tar 20 Agosti,2015 Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia kombe la kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi,Tarehe 8 Agosti,2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya kwa ofisi hiyo kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi,Tarehe 8 Agosti,2015.

Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Francis Mutungi akipata maelezo ya bidhaa zinazotengezwa na wajasiriamali kutoka Zanzibar waliowezeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko,Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF)na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu,Flora Mazilengwe, walipotembelea banda hilo Tarehe 8 Agosti,2015.

Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Fadhili Mtengela akieleza uratibu wa shughuli za maafa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnolela walipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi,Tarehe 8 Agosti,2015.

Mtaalamu kutoka Mradi wa MIVARF,Betha Mjawa akifafanua shughuli za mradi huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruhangwa,Mariam Mtima alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi,Tar 5 Agosti,2015.

Mkuu wa Wilaya ya Ruhangwa,Mariam Mtima akisisitiza jambo alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi,Tar 5 Agosti,2015.wa kwanza kulia ni Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Regina Kikuli.

Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Fadhili Mtengela akieleza uratibu wa shughuli za maafa kwa wananchi waliotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi,Tar 5 Agosti,2015.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Maria de Mattias wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda la Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kutembelea Idara zilizoshiriki katika maonesho ya Nane Nane tarehe 04 Agosti,2015 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Yokobetty Malisa (wa kwanza kulia) akieleza majukumu ya Idara hiyo kwa wanafunzi wa kidato cha pili kutoka shule ya Sekondari ya Maria de Mattias walipotembelea Idara hiyo Agosti 4, 2015 wakati wa maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Dodoma.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho ya Sherehe za Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikuli (wa kwanza kushoto) akimsikiliza mwanakikundi cha Mkombozi kata ya Masanga wilayani Kishapu Shinyanga wakati akieleza manufaa ya ufugaji wa mbuzi waliowapata kupitia Mradi wa kupunguza Athari za Maafa ya Ukame wilayani Kishapu Shinyanga, tarehe 5 Julai,2015. Kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi hiyo, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikuli akiongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya wakati wa kufuatilia Utekelezaji wa Mradi wa kupunguzaAthari za Maafa ya Ukame kijijini Masanga , wilayani Kishapu Shinyanga, tarehe 5 Julai, 2015, Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia UNICEF.

Mwanakijiji cha Uzogore,Mkoani Shinyanga,akitumia mawe kufafanua uwiano wa Hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani humo wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 28, Juni, 2015

Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe nchini katika kijiji cha Uzogore mkoani Shinyanga, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 28, Juni, 2015.

Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akifafanua juu ya Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe nchini wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga walipokuwa wakijifunza uendeshaji wa tathmini hiyo katika kijiji cha Uzogore mkoani humo tarehe 28, Juni, 2015.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia kombe la Ushindi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika masuala ya Uratibu na Usimamizi wa masuala ya Ukimwi wakati wa kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma tarehe 23 Juni, 2015.

MINISTERS IN THE PRIME MINISTER'S OFFICE

Hon.Hawa Abdulrahman Ghasia(MP) Minister of State (Regional Administration & local government)

Hon. Jenista Joakim Mhagama(MP). The Minister of State (Policy, Coordination & Parliamentary )

Hon. Eng. Christopher Kajoro Chiza(MP) Minister of State (Investment and Empowerment)

Video

Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday42
mod_vvisit_counterYesterday129
mod_vvisit_counterThis week678
mod_vvisit_counterLast week847
mod_vvisit_counterThis month1039
mod_vvisit_counterLast month3912
mod_vvisit_counterAll days333710
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved