Habari
Waziri Mhagama awapa kongole banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama afurahishwa na ushiriki wa ofisi yake katika uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani yanaendelea katika Viwanja vya Standi ya Zamani Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Maonesho hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambapo yameambatana na uwepo wa maonesho mbalimbnali, shughuli za uzalishaji katika kuipamba wiki ya vijana inayozinduliwa tarehe 10 Oktoba, 2023 Wilayani humo Mkoani Manyara.
Waziri Mhagama amepongeza maandalizi yaliyofanywa na kuendelea kuisihi ofisi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu uwepo wa mvua za El nino nchini kwa kuzingatia utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
=MWISHO=