Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Watendaji wahimizwa kuongeza kasi utekelezaji wa Mradi wa AFDP


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza kuwa na vikao vya uratibu vya pamoja kati ya wizara na taasisi zinazotekeleza mradi wa mradi wa AFDP ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.  George Simbachawene alipotembelea shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es salaam ambalo linatekeleza programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi katika mradi wa AFDP unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu na kutekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Zanzibar.

Waziri Smbachawene amesema programu AFDP ni ya miaka sita kuanzia 2021/2022 hadi 2027/2028 ambayo itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani 77.4 millioni (Mkopo toka IFAD USD 58.8 millioni; Serikali USD 7.7 millioni; Sekta Binafsi 8.4 millioni na Wananchi USD 2.4 millioni).

 “Mradi huu wa  uchumi wa bluu ukisimamiwa vizuri utaibua shirikia la TAFICO, na utaibua uchumi wa biashara ya uvuvi zinazofanywa na sekta binafsi.“

Lazima tutengeneze kikosi kazi kitakachokuwa kinaashughulikia changamoto zinazojitokeza kutoka taasisi moja kwenda nyingine pamoja na wizara moja kwenda nyingine katika utekelezaji wa mradi, alisema Waziri.

“Eneo hili linaloshughulikiwa na shirika la TAFICO linaenda kujibu ahadi za ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.”

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema mradi huu ni mradi mkubwa sana na ni mradi wa kimkakati.

“Tuone namna ambavyo tutautekeleza huu mradi kikamilifu, spidi na kasi ya utekelezaji wa mradi bado hairidhishi.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shirika la TAFICO Profesa Yunus Mgaya amesema wanalichukulia shirika la TAFICO kama shirika la kimkakati hasa katika dhana ya kutekeleza uchumi wa blue.

“Shirika linajukumu la kuwasaidia wavuvii wadogo wadogo hasa katika kunyanyua  vipato vyao, kuwawezesha kuhifadhi mazao yao ya uvuvi kuingia ubia na wananchi mbalimbali katika shughuli za uvuvi bahari kuu,”