Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi wakutuna na Katibu Mkuu Dkt. Yonazi


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amekutana na ujumbe kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya AFDP pamoja na Wataalam na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma Mei 9, 2023.

Katika Mazungumzo yao, Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alieleza kuwa Serikali tayari inatoa ushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza program hiyo na pia, kwa wakati inaainisha masuala mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika utekelezaji wake na kutafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu za Serikali.

Kwa Upande wake, Mwakilishi Mkazi wa program hiyo nchini Bw. Robson Mutendi alisema,ujumbe huu maalum wa ukaguzi wa maeneo ya mradi, utatembelea katika baadhi ya maeneo ambayo mradi unatekelezeka ikiwa ni njia mojawapo ya kuona na kuainisha maeneo yenye mapungufu, ili kufanyiwa kazi na kufikia malengo, na kuomba ushirikiano katika utendaji ili uweze kuleta matokeo tarajiwa.

Baada ya mazungumzo hayo mahususi na Katibu Mkuu, Ujumbe huo pamoja na wataalam utakutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi na pia utambelea baadhi ya maeneo inapotekelezwa program hiyo ikiwa ni pamoja na mikoa ya Tabora, Geita , Lindi na Zanzibar.

 

=MWISHO=