Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Uandaaji Utekelezaji wa Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini Kuongeza kasi ya Ukamilishaji wa Miradi ya Mendeleo Nchini


Imeelezwa kuwa zoezi la uandaaji Utekelezaji wa Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini Kunachangia kuongeza kasi ya Ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kuzingatia mchango wake katika kurahisisha shughuli za utekelezaji wa Miradi mbalimbali na kujiletea maendeleo nchini.

Haya yamezunguzwa na Dkt. James Henry Kilabuko Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu akizungumza kwa niaba ya Dkt. Jim Yonazi Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Wakurugenzi, Maafisa Mipango na Wakuu wa Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM), Mkoani Iringa.

Amesema, kikao hiki ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuimarisha mifumo ya usimamizi wa utendaji, uwajibikaji na kuhakikisha kuwa Afua mbalimbali za Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi kwa wakati.

Aidha amesema Ofisi ya Waziri Mkuu, ikiwa na jukumu la kikatiba la kuratibu na kusimamia utendaji wa shughuli za Serikali, imeona ni muhimu kukutana ili kujadili kwa kina dhana ya Ufuatiliaji na Tathmini ikiwa na utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya Ufuatiliaji na Tathmini ikiwemo Muongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini uliotolewa Juni 2024.

"Ofisi ya Waziri Mkuu, iliandaa Muongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini, ili kutoa maelekezo elekezi na sanifu yatakayowezesha Serikali kufuatilia, kutathmini na kupima utendaji wa taasisi zote kwa pamoja, kwa kutumia dhana ya "The Whole of Government Approach" Amesema Dkt. Kilabuko

Aidha amewasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuhakikisha suala la Ufuatiliaji na Tathmini linafanyika kwa ufanisi na ni wajibu wa Wakurugenzi kuhakikisha kwamba Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmin vilivyoanzishwa mwezi Aprili 2024, vinapewa rasilimali watu na fedha za kutosha, na vinapata ushirikiano kutoka idara zote.

Pia amewataka maafisa Mipango wote nchini Kuhakikisha mipango wanayoiandaa na kuratibu inakwenda sambamba na viashiria vya Ufuatiliaji na Tathmin tangu hatua za awali.

Mwisho  amewatakia mafanikio washiriki wote wa kikao kazi hicho na kuwasihi kutumia vizuri muda uliotengwa kwa tija na kujenga mtandao baina yao kwani Serikali tayari imeshaonesha njia na itaendelea kuwaunga mkono katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

 

=MWISHO=