Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Tanzania yashiriki kwenye Mkutano wa maswala ya Hali ya Hewa na usimamizi wa maafa Kusini mwa Afrika


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliolenga kuhusu namna ya kuchukua tahadhari za mapema katika hatua za Kudhibiti Majanga.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza tarehe 08-09/092022 umedhaminiwa na UN World Materological Organisation na unafanyika Mjini Maputo Nchini Msumbiji Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa wataalamu wa maswala hayo ulioanza 05-07/09/2022.