Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Suala la maafa ni la kila mmoja, jamii yaaswa kuchukua tahadhari.


Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhali za kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea hasa kwa kipindi hiki cha mvua za Vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Disemba, 2023 kwa kuhakikisha wanahama sehemu hatarishi na maeneo yote yanayoweza kuleta madhara yanatunzwa ipasavyo ili kuendelea kulinda mali na makazi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Bw. Prudence Constantine wakati wa kongamano na maonesho yanayoendelea ya wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika Jijini Arusha ambapo Idara hiyo imepata fursa ya kutoa elimu kwa umma juu ya kujikinga na kukabiliana na Maafa.

Aidha Bw. Prudence amesema hadi sasa Wananchi kupitia ngazi mbalimbali wamesha pelekewa mpango utakaowawezesha kukabiliana na hali hiyo na waweze kuchukua tahadhali madhubuti.

“Japokuwa Serikali imeshaanza kutoa elimu kwa Umma na imezungumza na vyombo vya habari pamoja na kutoa mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na madhara yanayoweza kutokana na mvua za El-Nino, kwa upande wetu idara ya menejimenti ya maafa tukaona ndani ya kongamano hili tuweze kushiriki ili kutoa elimu kwa wananchi pamoja na njia gani watakavyoweza kukabili jambo hilo litakapotokea”.alisema Prudence

Hivi karibuni Mamlaka ya hali ya hewa walitanganza kuwepo kwa   Mvua za El-Nino za juu ya wastani kwa mikoa 14 ikiwa kati ya mikoa hiyo Mkoa wa Arusha ni Miongoni mwa Mikoa hiyo. 

=MWISHO=