Habari
Rasimu ya Mwongozo Jumuishi wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmin Wajadiliwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kupitia Rasimu ya Mwongozo Jumuishi wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini Kilichofanyika tarehe 28 Februari, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano Ngome Jijini Dodoma.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa Vitengo vya Ufuatili na Tathmin pamoja na Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Ofisi ya Waziri Mkuu.