Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Rais Dkt.Samia aongoza Watanzania kuaga Mwili wa Hayati Cleopa Msuya


Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongoza Watanznai kuaga Mwili wa Hayati Cleopa David Msuya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ibada maalum ya kumuombea katika Viwanja vya Karimjee tarehe 11 Mei, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa dini,Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na nje ya mkoa huo.

Hayati Msuya anaatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro tareeh 13 Mei, 2025.

 

=MWISHO=