Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Ofisi ya Waziri Mkuu yaibuka mshindi wa Kwanza kwa ubora Sabasaba 2024


Ofisi ya Waziri Mkuu yaibuka mshindi wa kwanza kwa banda bora na utoaji bora wa huduma kwa ngazi ya Wizara zilizoshiriki katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.

Akipokea tuzo ya Ofisi hiyo kwa niaba ya Uongozi wa Ofisi, Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Condrad Millinga ameshukuru kwa namna ushindani ulivyoenda na kuipa Ofisi ya Waziri Mkuu ushindi wa Kwanza katika maonesho hayo.

Amepokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Sulemani Jafo hii leo Julai 13, 2024

Maonesho hayo yamefungwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ambapo yalikuwa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na  Uwekezaji,"

 

=MWISHO=