Habari
Meja Jenerali Mbuge: Tutumie rasilimali zilizopo kukabili maafa
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Meja Jenerali Charles Mbuge ameiasa jamii kuendelea kutumia rasilimali zilizopo katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kujionesha shughuli zinazoendelea katika banda la Ofisi yake katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Meja Jenerali Mbuge alisema kuwa ni muhimu kuendelea kujiandaa na kujilinda na maafa kwa kutumia rasilimali zilipo nchini ili kuwa na mazingira salama na bora katika nchi yetu.
“Tutumia rasilimali tulizonazo katika masuala haya ya maafa kwa kuzingatia masuala ya usimamizi wa maafa ni jukumu la kila mmoja katika eneo lake huku tukizingatia maelekezo ya kitaalam ya usimamizi wa maafa nchini,”alisema
Aidha alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya majanga na tahadhali zinazotolewa na Mamlaka husika ili kuwa na utaratibu wa kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.
=MWISHO=