Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Katibu Mkuu Dkt. Yonazi aongoza Kikao cha Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM)


Kikao cha wajumbe wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa programu za Malaria, Kifua Kikuu, Malaria, UKIMWI na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji wa Huduma za Afya kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia. Kikao hicho kilifanyika tarehe 24 Agosti 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Serengeti uliopo Jengo la Ushindani , Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalaum, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Sekretarieti ya TNCM, Asasi za Kiraia (Non State Actors - NSAs) na Wadau wa Maendeleo ambapo kiliongozwa na Dkt. Jim James Yonazi, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye pia nidye Mwenyekiti wa TNCM.

kimejadili hatuaya utekelezaji wa programu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia ikiwemo mafanikio na changamoto zinazoathiri utekelezaji wa programu hizo pamoja na kujadili mikakati ya kukabiliana nazo.

 

=MWISHO=