Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Jitokezeni kwenye zoezi la sensa ili muhesabiwe


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu  Mhe. George  Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.

“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla”

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene baada ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa lile fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agusti 2022, alisema  Waziri”