Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna kwa lengo la kumpitisha katika majukumu yanayohusu taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya ratiba ya Katibu Mkuu huyo kujengewa uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara na Taasisi zilizochini ya Ofisi yake.

Kikao hicho kilifanyika Machi 10, 2023 katika ofisi yake Jijini Dodoma na kueleza kuwa ofisi yake itaendela kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele nchini na yanaratibiwa kwa matokeo chanya.