Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Habari

Dkt. Biteko ashiriki Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  Julai 25, 2025 ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma,

Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi mbalimbali wameshiriki katika maadhimisho hayo wakiwemo viongozi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na Viongozi wa Dini.