Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Wasifu

Mh. Salim Ahmed Salim
Mh. Salim Ahmed Salim
Waziri Mkuu Mstaafu

Waziri Mkuu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Edward M. Sokoine ambaye alifariki kwa ajali ya gari mnamo tarehe 12 Aprili, 1984. Ni mwanadiplomasia wa siku nyingi kuanzia miaka ya 1960. Alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 24 Aprili, 1984 hadi tarehe 5 Novemba, 1985 akifuatiwa na Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba.