Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA WAZIRI MKUU

Wasifu

Mh. Cleopa David Msuya
Mh. Cleopa David Msuya
Waziri Mkuu Mstaafu

Waziri Mkuu wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea nafasi hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Edward M. Sokoine. Aliwahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu mara mbili. Mara ya kwanza ni kuanzia tarehe 7 Novemba, 1980 hadi tarehe 24 Februari, 1983. Mara ya pili ilikuwa ni tarehe 5 Desemba, 1994 hadi tarehe 28 Novemba, 1995 huku akishika pia wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sasa, ameshastaafu siasa ingawa bado anashika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Taasisi mbalimbali za Jamii.