HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA UFUNGUZI WA MICHEZO YA SHIRIKISHO LA MAJESHI YA POLISI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI KWENYE UWANJA WA UHURU JIJINI DAR-ES-SALAAM TAREHE 6 AGOSTI, 2018

Mhe. Eng. Hamad Masauni (Mb),Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

Ndg. Simon N. Sirro, InspektaJeneraliwa Polisi Tanzania;

Wakuu waVyombovyaUlinzi na Usalama;wakiwemo

Mkurugenzi Mkuu waTaasisi ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa Tanzania,

Ndg. Martin OkothOchola, Mwenyekiti waEAPCCO na InspektaJenerali wa Polisi wa Uganda;

Ndg. GidionKimilu, Mkuu wa INTERPOL Kanda ya Mashariki (EAPCCO);

WaheshimwaMabaloziwa Nchi zinazoshiriki Michezo;

Wakuu waMisafara wa Nchi Wanachama wa EAPCCO mlioko hapa;

MaofisaWaandamizi kutoka Jeshi la Polisi kote Afrika Mashariki;

Wageni Waalikwa;

Wanamichezowa Michezo wote;

NduguWanahabari;

MabibinaMabwana.

Nianze kwakumshukuruMwenyeziMungu ambaye ametuwezeshasotekuja hapa natambuakuwa kuna nchi zote za Afrika Mashariki wanachama wake na majeshiyoteyako hapa Tanzania. Lakininimshukurusana Naibu waziri wa Nchi wa mambo ya ndani kupitia Jeshi lake la Polisi kwa maamuzi yao ya kuandaatukiokubwamuhimu ambalo nitalizinduamudamfupiujao.Aidha,nimshukuruKamanda Simon Sirro, InspektaJeneraliwa Polisi kwa kunialika kuwa MgeniRasmiambapo angewezakumualikayeyotekatika ufunguzi wa michezo hii. Nakushukurusana!

Kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais waSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba yaWatanzania wote na kwa niabayangu binafsi, napenda kutumia fursa hiikuwakaribishamakamanda wote mliotoka kwenye nchi zote za Afrika Mashariki. Karibunisana Tanzania!

Kama ambavyommekuwamkisikiakutoka kwenye vyanzombalimbalikuhusuutulivu na amani iliyopo nchini kwetu Tanzania, leo hiimnashuhudiawenyewe tangu kuwasili nchini kwetukwambaTanzania bado ni nchi salama na watanzania ni wakarimu na naamini katika kipindimtakachokuwepo hapa mtabaki kuwa salama.

Ndugu wageni, viongozinaMakamandawa Jeshila Polisi Afrika Mashariki

Niwakaribishetenajijini Dar es Salaam nyoteambaommekuja hapakushiriki michezo hii ya majeshi ya jeshi la polisi Afrika Mashariki. Lengo letu la michezo hiinikuhakikishakwambatunaunganisha nguvu za pamoja za kiulinzi na kiusalama kwenye ukandawetu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hivyotutaendeleakutumia fursa hii kuimarisha mshikamanowetukwakuwaunganishavijanawetu kupitia michezo ili kila mmoja awezekuwajibika kwenye jambokuu la ulinzi kwenye nchi zetu za Afrika Mashariki.

Ndugu wageni, viongozinaMakamanda wa Jeshi la Polisi Afrika Mashariki

Leo hiindiosiku ya uzinduziwa michezo yetu ya majeshi ya Jeshila Polisi Afrika Mashariki EAPCCO hapa Tanzania.

Kwa namna ya pekee, nimpogezeInspektaJeneraliwa Polisi, Ndg. Simon Sirro kwa kitendochake cha kukubalikuwa mwenyeji wa michezo hii ya Awamu ya Pili baada ya ile ya Awamu ya Kwanza iliyofanyika nchini Uganda mwaka jana. Kukubalikwenu michezo hiiifanyike hapa nchini Tanzania, Serikali tumefurahishwasana na tutaendeleakuwapaushirikianowakati wote wa michezo hii hapa nchini Tanzania.

Ndugu wageni, viongozinaMakamanda wa Jeshi la Polisi Afrika Mashariki

Nitoewitokwenukuendelezaushirikianouliopobaina ya nchi wanachama waShirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki katika nyanjambalimbaliikiwemokukabiliana na uhalifuunaovukamipaka hususan katika ukandawetu wa Afrika Mashariki. Tabiahii ya kushirikiana kupitia michezo inastahilikupongezwakwaninihatuamuhimukatika kuimarishaushirikianona hivyo, kuwezeshamapambanodhidi ya uhalifuunaovukamipaka kwa pamoja. Na kwaushirikianohuu,inaoneshammetafuta njia nzuri ya kuimarisha mshikamano.

Natakakuwahakikishiakwamba nchi zetuzitakuwasalamapindimtakavyokuwammemaliza michezo hiiambayotunaaminimtaitumia pia kama sehemu ya kujadili na kubadilishanamawazo ya njia nzuri ya kuimarisha ulinzi kwenye maeneoyetu.  Malengoyetukwa pamoja ni kuhakikishakwambaukandawetu wa Afrika Mashariki unabakisalama na unakuwa wa amani na kilamwanajamiianawezakutumia fursa zilizopoakiwasalama.

Hivyoniwapongezewanamichezo wote ambao pia mmepatanafasi ya kuwakilishamajeshiyenukuja hapa Tanzania kwenye mashindano haya, na kwa nafasihiiniwapongeze wote waliowezeshamaandalizi ya michezo hiikufanikiwa na kufikiahatuahii ya uzinduzi.

Lakinitukumbuke kuwa tabia ya michezo inakuwanamatokeomatatuambayoyanaweza kuwa kushinda, kushindwa na kutoka sare ni vemakila mmoja akajiandaakisaikolojia kwa lolotelinalowezakutokea kwenye michezo yetu. Jambojema kwa wanamichezo nikufahamu kuwa lengo sikupataushinditubalinikuimarishaushirikianowetu hasa katika nyanja za kupambana na kuzuiauhalifu, tukifanikiwakuzuiauhalifu na kufanya ukandawetu kuwa sehemu ya amani hapondipotutakuwatumefanikiwakufikiamalengo ya shirikishohililililoundwa na Makamanda Wakuu wa Jeshila Polisi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

KAULIMBIU YA MASHINDANO

Ndugu wageni, viongozinaMakamanda wa Jeshi la Polisi Afrika Mashariki

Nimefurahishwanakaulimbiu ya michezo hiiisemayo:“Michezo katika Kukuza Ushirikiano wa Kikanda wa Polisi, Amani na Usalama”.(Sports for Promoting Police Regional Cooperation, Integration, Peace and Security).Kaulimbiu ya michezo hiiinajielezayenyewekuhusuumuhimuwa kushirikiana katika kuleta amani na usalama.

Wote tunaelewa kuwa makosayanayovukamipakakama vile vitendovyaugaidi, ujangili, usafirishajiharamu wa binadamu, biasharaharamu ya silahandogondogo na nyepesi, bidhaabandia na hafifu, utakatishaji wa fedhaharamu, biashara ya dawa za kulevya na mienendo ya wahalifuwanaovukamipakahuathiri amani, usalamana maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kandayetu. Uhalifuhuuhauwezikuzuiwapasipojitihada za makusudinamikakati ya pamoja ya kupambanaambayonyiewakuu wa majeshi ya polisi ya Afrika Mashariki mnaipanga.

MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU

Ni matarajioyangu kuwa michezo hiiitatoa fursa ya kipekeekwanchi wanachama kubunimikakatimbalimbali ya kupambana na kuzuiauhalifu hasa uleunaovukamipaka ya nchi zetu. Tutumie fursa hii katika kubadilishanataarifa za kiintelijensia, kujadilinamna ya kufanya operesheni za pamoja na kwa wakati mmoja na pia namna ya kushirikiana katika masuala ya kisheriaambayomaranyingiyamekuwavikwazo katika utendajiwetu hasa katika shughuli za upelelezi ili kuendeleakuwatiahatianiwahalifuwanaovukamipaka.

HITIMISHO

Ninayoimani kuwa mwisho wa michezo hiihatutokuwatumepatawashindipekeyakebalipia tutakuwatumeimarishaumoja naushirikiano katika kukuza amani na usalamahukutukiendeleakupambana na uhalifuunaovukamipaka ya nchi yetu. Na hapondipotutakuwatumetimiza lengo la Shirikisho la Wakuu wa Polisi la Ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa kufanya hivyo,tutakuwa kwenye nafasinzuri yakuendelezamaendeleo ya kiuchuminakijamiiambayoyameanzakuonekana katika nchi zetu.

Hivyonibudikupelekaujumbe kwa raia kuwa jeshi la polisi linahitajikuungwamkono katika jitihadazake za ulinza na usalamakote Afrika Mashariki. Kwa kumalizia napenda tenakutumia fursa hiikuwakaribisha wote nchini pamoja nakukumbusha kuwa Tanzania ina fursa nyingi na vivutiovingiikiwemomaeneomengi ya kutembelea, hivyomtakapomaliza michezo mnawezakubakikidogo na kutembeleamaeneohayo.

Niwatakie michezo mizuriyenye amani, iliyohuruna haki,hukutukikumbuka kuwa michezo ni moja ya nyenzo ya kuleta amani na usalama katika jamiizetu. Baada ya kusemahayo, sasa napenda kutamka kuwa Awamu ya Pili ya Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukandawa Afrika Mashariki imefunguliwarasmi.

Ahsantenisana kwa kunisikiliza.