WAZIRI MKUU ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU RUANGWA

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumatano, Julai 15, 2020) amechukua fomu ya kuwania tena ubunge wa jimbo la Ruangwa, wilayani humo, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye alizijaza fomu hizo akiwa ofisini hapo na kuzirudisha kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Barnabas Essau, pia alilipa fedha taslimu sh. 100,000 zikiwa ni ada ya kuchukua fomu hizo.

Waziri Mkuu aliambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitoa ratiba ya kuwapata wagombea ubunge, udiwani na viti maalumu kwa ajili ya uchanguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo wagombea wa nafasi hizo walitakiwa kuchukua fomu kuanzia Julai 14, 2020 na kuzirejesha Julai 17, mwaka huu saa 10.00 jioni.

-ends-