Home | Speech
Speech
Speeches

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

Hotuba ya Mheshimiwa Mizengo P. Pinda (Mb) Waziri Mkuu Wakati wa Kufungua Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu vya Dodoma katika Ukumbi wa African Dreams – Dodoma, tarehe 25 Juni 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji Getrude Nyaulawa ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Kawe jijini Dar es salaam November 11,2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

HOTUBA YAMHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA AKIJIBU HOJA ZA WABUNGE KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011

 
 

UTANGULIZI

 

 

Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha na kunipa afya njema hadi jioni ya leo ninapohitimisha majadiliano ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini ya Waziri Mkuu pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2010/2011.

 
 

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana wewe mwenyewe, Naibu Spika na Wenyeviti wote kwa kusimamia kwa umakini mkubwa majadiliano ya Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake. Niwashukuru pia Waheshimiwa Wabunge wote kwa namna ya pekee kwa michango yenu ya kina ambayo imefanikisha kwa kiasi kikubwa kazi ambayo ilikusudiwa tuifanye.

 
 

WACHANGIAJI

 

 

Mheshimiwa Spika, katika mjadala huu jumla ya Waheshimiwa Wabunge 179 walichangia, Waheshimiwa Wabunge 70 walichangia kwa kuzungumza moja kwa moja hapa Bungeni na Wabunge 109 wamechangia kwa njia ya maandishi.

 
 

Mheshimiwa Spika, hoja ni nyingi tumejitahidi kujibu baadhi na zimebaki nyingi. Wizara nazo zimejitahidi kujibu lakini na wenyewe hawakuweza kumaliza zote, matumaini yangu ni kwamba wataziendeleza wakati wakiwasilisha hotuba za bajeti zao.

 
 

Mheshimiwa Spika, hata baada ya kufanya hivyo, bado naamini hoja nyingi zitaendelea kubaki. Nataka niahidi Bunge lako tukufu kwamba hoja zote hizi kwa ujumla wake zitaandaliwa katika maelezo ya maandishi na zitagawiwa kwa Waheshimiwa Wabunge.

 
 

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo niruhusu kwanza niwatambue Waheshimiwa waliochangia kwa kuzungumza hapa Bungeni na wale waliochangia kwa maandishi kama ifuatavyo;

 
 

Waliochangia kwa kuzungumza;

 
 

Mheshimiwa George M. Lubeleje Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mheshimiwa Dkt. Wilbroad P. Slaa Msemaji wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Karatu, Mheshimiwa Anne K. Malecela Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa Castor Raphael  Ligallama kutoka Kilombero, Mheshimiwa Diana M. Chilolo Viti Maalum, Mheshimiwa Anna Margareth Abdallah Viti Maalum, Mheshimiwa Mkiwa A. Kimwanga Viti Maalum, Mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu Kuteuliwa, Mheshimiwa Dkt. Charles O. Mlingwa Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Haroub Said Masoud Mbunge wa Koani na Mheshimiwa Gosbert B. Blandes Mbunge wa Karagwe.

 
 

Mheshimiwa John P. Lwanji Mbunge wa Manyoni Magharibi, Mheshimiwa Vedastus M. Manyinyi Mbunge wa Musoma Mjini, Mheshimiwa Magdalena H. Sakaya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Grace S. Kiwelu Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Dkt. Luka Jelas Siyame Mbunge wa Mbozi Magharibi, Mheshimiwa Prof. Philemon N. Sarungi Mbunge wa Rorya, Mheshimiwa Godfrey W. Zambi Mbunge wa Mbozi Mashariki, Mheshimiwa Omar S. Kwaangw’ Mbunge wa Babati, Mheshimiwa Mwichoum A. Msomi Mbunge wa Kigamboni na Mheshimiwa Paschal C. Degera Mbunge wa Kondoa Kusini.  

 
 

Mheshimiwa Victor K. Mwambalaswa Mbunge wa Lupa, Mheshimiwa Riziki Said Lulida Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Lediana M. Mng’ong’o Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Abdulkarim Esmail Hassan Shah Mbunge wa Mafia, Mheshimiwa Lucas L. Selelii Mbunge wa Nzega, Mheshimiwa Halima J. Mdee Viti Maalum, Mheshimiwa Abbas Z. Mtemvu Mbunge wa Temeke, Mheshimiwa Jacob D. Shibiliti Mbunge wa Misungwi na Mheshimiwa Aziza S. Ally Mbunge Viti Maalum.

 
 

Mheshimiwa Said Nkumba Mbunge wa Sikonge, Mheshimiwa Dkt. Haji Mwita Haji Mbunge wa Muyuni, Mheshimiwa Riziki Omar Juma Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim Mtambile, Mheshimiwa Halima O. Kimbau Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Florence E. Kyendesya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Michael L. Laizer Mbunge wa Longido, Mheshimiwa Jackson M. Makwetta Mbunge wa Njombe Kaskazini na Mheshimiwa Lucy F. Owenya Mbunge Viti Maalum.

 
 

Mheshimiwa Mwanawetu S. Zarafi Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Mchungaji Lucksona Ndaga Mwanjale Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mheshimiwa Shally J. Raymond Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Mohamed H. Missanga Mbunge wa Singida Kusini, Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Dkt. Juma A. Ngasongwa Mbunge wa Ulanga Magharibi, Mheshimiwa Aloyce B. Kimaro Mbunge wa Vunjo, Mheshimiwa Mwanne I. Mchemba Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo Mbunge wa Tandahimba na Mheshimiwa Hasnain G. Dewji Mbunge wa Kilwa Kusini.  

 
 

Mheshimiwa Bujiku P. Sakila Mbunge wa Kwimba, Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Eustace O. Katagira Mbunge wa Kyerwa, Mheshimiwa Janeth B. Kahama Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Abdul Jabir Marombwa Mbunge wa Kibiti, Mheshimiwa Kaika Saing’o Telele Mbunge wa Ngorongoro, Mheshimiwa Hamza A. Mwenegoha Mbunge wa Morogoro Kusini, Mheshimiwa Dkt. Samson F. Mpanda Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Mheshimiwa Zuleikha Yunus Haji Mbunge Viti Maalum na Mheshimiwa Zaynab M. Vullu Mbunge Viti Maalum.

 
 

Mheshimiwa Christopher O. Ole-Sendeka Mbunge wa Simanjiro, Mheshimiwa Fuya G. Kimbita Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Tatu M. Ntimizi Mbunge wa Igalula, Mheshimiwa Martha M. Mlata Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Prof. Jumanne A. Maghembe Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Prof. David H. Mwakyusa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Dkt. Shukuru J. Kawambwa Waziri wa Miundombinu, Mheshimiwa Phillip S. Marmo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mheshimiwa Aggrey D. J. Mwanri Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, na Mheshimiwa Celina O. Kombani Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI

 
 

Wachangiaji kwa Maandishi

 

 

Mheshimiwa Spika, waliochangia kwa maandishi ni hawa wafuatao;

 
 

Mheshimiwa Jackson M. Makwetta Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mheshimiwa Savelina Silvanus Mwijage Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Eng. Stellah M. Manyanya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Balozi Getrude I. Mongella Mbunge wa Ukerewe, Mheshimiwa Samuel M. Chitalilo Mbunge wa Buchosa, Mheshimiwa Herbert J. Mntangi Mbunge wa Muheza, Mheshimiwa Mwadini Abbas Jecha Mbunge wa Wete, Mheshimiwa Hemed Mohammed Hemed Mbunge wa Chonga, Mheshimiwa Dkt. Samson F. Mpanda Mbunge wa Kilwa Kaskazini na Mheshimiwa Ahmed Mabkhut  Shabiby Mbunge wa Gairo.  

 
 

Mheshimiwa Dkt. Abdallah O. Kigoda Mbunge wa Handeni, Mheshimiwa Brig. Jen. Hassan Athuman Ngwilizi Mbunge wa Mlalo, Mheshimiwa Mussa A. Zungu Mbunge wa Ilala, Mheshimiwa Ephrahim N. Madeje Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Mwanne I. Mchemba Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Prof. Peter Mahamudu Msolla Mbunge wa Kilolo, Mheshimiwa Mossy Suleiman Mussa Mbunge wa Mfenesini, Mheshimiwa Dkt. Binilith S. Mahenge Mbunge wa Makete, Mheshimiwa Anne K. Malecela Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa Martha Jachi Umbulla  Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Godfrey W. Zambi Mbunge wa Mbozi Mashariki na Mheshimiwa Mwinchoum A. Msomi Mbunge wa Kigamboni.

 
 

Mheshimiwa Basil P. Mramba Mbunge wa Rombo, Mheshimiwa Andrew J. Chenge Mbunge wa Bariadi Magharibi, Mheshimiwa Eng. Fuya G. Kimbita Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Dorah H. Mushi Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Omar Ally Mzee Mbunge wa Kiwani, Mheshimiwa Juma H. Killimbah Mbunge wa Iramba Magharibi, Mheshimiwa Hamza A. Mwenegoha Mbunge wa Morogoro Kusini, Mheshimiwa Mbaruk Kassim Mwandoro Mbunge wa Mkinga, Mheshimiwa William H.Shellukindo Mbunge wa Bumbuli, Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Pindi Hazara Chana Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Said Msabaha Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mheshimiwa Nuru Awadh Bafadhil Mbunge Viti Maalum na Mheshimiwa James D. Lembeli Mbunge wa Kahama.

 
 

Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim Mbunge wa Mtambile, Mheshimiwa Rajab Ahmad Juma Mbunge wa Tumbatu, Mheshimiwa Gosbert B. Blande Mbunge wa Karagwe, Mheshimiwa John P. Lwanji Mbunge wa Manyoni Magharibi, Mheshimiwa Mathias M. Chikawe Mbunge wa Nachingwea, Mheshimiwa Jacob D. Shibiliti Mbunge wa Misungwi, Mheshimiwa Mgana I. Msindai Mbunge wa Iramga Mashariki, Mheshimiwa Ameir Ali  Ameir Mbunge wa Fuoni, Mheshimiwa Omar Shaaban Kwaangw’ Mbunge wa Babati Mjini na Mheshimiwa Col. Feteh Saad Mgeni Mbunge wa Bumbwini na Mheshimiwa Ali Khamis Seif  Mbunge wa Mkoani.

 
 

Mheshimiwa Riziki O. Juma Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Gideon A. Cheyo Mbunge wa Ileje, Mheshimiwa Mariam R. Kasembe Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu Mbunge wa Kuteuliwa, Mheshimiwa Dkt. Harrison G. Mwakyembe Mbunge wa Kyela, Mheshimiwa Dkt. Maua A. Daftari Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Fatma Abdalla Tamim Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Janeth Mourice Massaburi Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Prof. Raphael B. Mwalyosi Mbunge wa Ludewa na Mheshimiwa Mkiwa A. Kimwanga Viti Maalum.  

 
 

Mheshimiwa Joyce M. Masunga Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Dkt. Luca Jelas Siyame Mbunge wa Mbozi Magharibi, Mheshimiwa Mohammed Habib Juma Mnyaa Mbunge wa Mkanyageni, Mheshimiwa Zaynab M. Vullu Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Kiumbwa Makame Mbaraka Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Bakar Shamis Faki Mbunge wa Ole, Mheshimiwa Esther K. Nyawazwa Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Paschal C. Degera Mbunge wa Kondoa Kusini na Mheshimiwa Diana M. Chilolo Mbunge Viti Maalum.  

 
 

Mheshimiwa Felister A. Bura Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Lucas L. Selelii Mbunge wa Nzega, Mheshimiwa Prof. Jumanne A. Maghembe Mbunge wa Mwanga, Mheshimiwa Juma Said Omar Mbunge wa Mtambwe, Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve, Mheshimiwa Halima O. Kimbau Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Mwanawetu Said Zarafi Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Dkt. Batilda Salha Burian Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Victor K. Mwambalaswa Mbunge wa Lupa, Mheshimiwa Lucy F. Owenya Mbunge Viti Maalum na Mheshimiwa Shoka Khamis Juma Mbunge wa Micheweni.

 
 

Mheshimiwa Bujibu P. Sakila Mbunge wa Kwimba, Mheshimiwa  Mustafa H. Mkulo Mbunge wa Kilosa, Mheshimiwa Abbas Z. Mtemvu Mbunge wa Temeke, Mheshimiwa John M. Cheyo Mbunge wa Bariadi, Mheshimiwa Bernadeta Kasabago Mushashu Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Loresia Bukwimba Mbunge wa Busanda, Mheshimiwa  Hasnain G. Dewji Mbunge wa Kilwa Kusini, Mheshimiwa Hadija Saleh Ngozi Mbunge wa Kuteuliwa, Mheshimiwa Fatma Othman Ali Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Salim Yussuf Mohamed Mbunge wa Koani, Mheshimiwa Khadija Salum Ally Al-Qassmy Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Castor R. Ligallama Mbunge wa Kilombero na Mheshimiwa Emmanuel Jumanne Luhahula Mbunge wa Bukombe.

 
 

Mheshimiwa Dkt. Mary M. Nagu Mbunge wa Hanang, Mheshimiwa Dkt. Lucy S. Nkya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Ussi Ame Pandu Mbunge wa Mtoni, Mheshimiwa Martha M. Mlata Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Mwajuma Hassan Khamis Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Kheri Khatib Ameir Mbunge wa Matemwe, Mheshimiwa Charles Muguta Kajege Mbunge wa Mwibara, Mheshimiwa Marim Salum Mfaki Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewa Mbunge Viti Maalum na Mheshimiwa Shally J. Raymond Mbunge Viti Maalum.  

 
 

Mheshimiwa Anastazia J. Wambura Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Tatu M. Ntimizi Mbunge wa Igalula, Mheshimiwa Halima M. Mamuya Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Teddy Louise Kasella-Bantu Mbunge wa Bukene, Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan Mbunge wa Kinondoni, Mheshimiwa Job Y. Ndugai Mbunge wa Kongwa na Mheshimiwa Clemence Beatus Lyamba Mbunge wa Mikumi.

 
 

Mheshimiwa Spika, inawezekana katika majina haya kuna mengine tumeyasahau kama tutakumbushwa basi tutalitambua vilevile.

 
 

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba muda wa kujadili bajeti ulikuwa mfupi, idadi hii kubwa ya wachangiaji inaonyesha jinsi ambavyo Waheshimiwa Wabunge mnavyoweka umuhimu katika majukumu yanayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake. Wote tunawashukuru sana.

 
 

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie fursa hii kuwashukuru waheshimiwa Wabunge wote kwa jinsi mlivyochambua kwa kina utekelezaji wa shughuli za Serikali. Mmefuatilia kwa karibu utekelezaji wa Serikali, mmedai taarifa mbalimbali na mmezijadili kwa lengo la kujiridhisha kuhusu ufanisi katika utendaji wake. Aidha, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali yake kwa kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Nawashukuru wote walioonyesha pale tulipofikia katika utekelezaji wake na pia niwashukuru wale wote walioonyesha maeneo ambayo hatukuweza kuyafikia kiutekelezaji. Kwangu mimi michango yote inatusaidia kufungua macho na kuona zaidi kile ambacho Wananchi wanategemea kutoka kwa Viongozi wao na Serikali yao kwa ujumla. Aidha, inatuonyesha kile ambacho Wananchi wamefanikiwa kupata na pale ambapo bado tunahitaji kupafanyia kazi.

 
 

Nitumie nafasi hii tena kuwashukuru wote kwa michango yao mmoja mmoja na kwa nia nzuri ya kulisaidia taifa letu na wananchi wake. Mimi ninaamini kwamba mijadala yote inatusaidia kujua maeneo ambayo tumefanya vizuri na yale ambayo hatukufanya vizuri tuendelee kujipanga tuweze kufanya vizuri. Aidha, kwa wote walioipongeza Serikali, pongezi hizo tutazitumia kuimarisha utendaji wetu wa kila siku na vilevile kwa Serikali yote kwa ujumla. Kwa ufupi nasema ahsanteni sana kwa ujumla wake.

 
 

HATUA YA MAENDELEO YALIYOFIKIWA TANGU UHURU

 
 

Mheshimiwa Spika, pamoja na shukurani hizo naomba pia uniruhusu nitoe angalau dukuduku langu moja kwa Watanzania wenzangu. Wako baadhi yao na wengine wamo humu Bungeni ambao wamekuwa kwa muda mrefu hivi wanadiriki kubeza baadhi ya juhudi ambazo Serikali imefanya hadi hivi sasa na kuonyesha kana kwamba hapa tulipo ni pabaya zaidi, duni zaidi, ni mahali panapotisha zaidi na panakatisha tamaa zaidi kuliko hata huko tulikotoka. Mimi binafsi siamini kuwa kauli hizi ni za dhati. Naelewa kuwa, wapo Watanzania waliozaliwa kabla ya uhuru, wako wa kipindi kati ya kupata Uhuru na Muungano, wako pia waliozaliwa kati ya Muungano na miaka ya 70, wako pia wa kizazi kipya.

 
 

Inawezekana kabisa kwa wale wote ambao hawakuzaliwa huko walikozaliwa hawa wazee waliotutangulia isiwe rahisi sana kuona tumetoka wapi na tunakwenda wapi na kwa bahati mbaya baadhi ya kauli hizi zinatoka hapa Bungeni kwa hiyo ndiyo kusema wako katika makundi haya. Kwa wale waliozaliwa baada ya miaka 70 ni dhahiri hawawezi kujua yaliyowasibu Wazee wa enzi hizo isipokuwa kwa kuelezwa au kusoma historia.

 
 

Hali kadhalika kwa waliozaliwa nyakati nyingine zilizofuata itakuwa hivyohivyo. Ni dhahiri kuwa kauli za namna hii, kwa muono wangu wakati mwingine zinavunja moyo, zinakatisha watu tamaa na zinafanya ionekane kana kwamba hakuna matumaini ya kwenda mbele. Lakini ukweli uliopo ni kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo na ninalisema hili kwa sababu hata wadau wetu wa maendeleo wanakubali kwamba Tanzania imefanya juhudi kubwa katika kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo. 

 
 

Nieleze basi angalau maeneo machache ambayo wote tungepaswa kuyakiri. Kwanza ni namna ambavyo Serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi imeweza kuiongoza nchi hii kwa kipindi chote hiki katika hali ya amani na utulivu mkubwa kabisa wa kisiasa. Leo tupo hapa tunajivuna kwa kuwa na demokrasia iliyopanuka, mfumo wa vyama vingi, uhuru mkubwa sana wa watu kwenda wanakotaka na kusema wanalotaka, umepanua sana wigo wa vyombo vya habari wakati mwingine watu wanafikiri kwamba pengine tumetoa uhuru kupita kiasi.

 
 

Pili, maisha ya wananchi. Nimekuwa najiuliza sana hivi ni kweli haya yanayosemwa? Hebu tazameni huduma za jamii nini kimefanyika? Hivi ni kweli kwamba wale waliokuwepo mwaka wa 1961 wakati wa uhuru hali ya huduma za Elimu zilikuwa kama zilivyo leo? Hali ya huduma za afya ni kweli zilikuwa kama zilivyo leo? Mimi siamini kama ni kweli. Tazameni hali ya miundombinu ilivyo nchini Tanzania sasa? Hivi ni kweli juhudi zote hizi ambazo zimefanyika si chochote, hakina maana na kwamba hakimsaidii Mtanzania? Mimi siamini hivyo!

 
 

Tazameni vilevile hatua tuliyopita katika matumizi ya TEKNOHAMA - mawasiliano yameongezeka, simu za mkononi zimeongezeka, sasa hivi mnazungumza internet na vitu vingine chungu nzima. Hivi ni kweli hakuna kilichofanyika kwamba hali ni bora kuliko ilivyokuwa siku za nyuma kuliko leo?

 
 

Mheshimiwa Spika, hata upeo wa Bunge lako ni tofauti kabisa na siku za nyuma. Mijadala ninayoisikia hapa na hoja zinazotolewa hapa, ni kielelezo tosha kwamba mliomo humu ni watu sasa ambao mmepea na mmepea kwa sababu wengi wenu mmesoma kutoka katika shule ambazo zimejengwa chini ya Serikali hii.

 
 

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nimejitahidi kujaribu kufanya mapitio ya mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya matumizi ya fedha za Ofisi yangu na ya Bunge, nimejaribu sana kutumia kipindi kirefu sana kujaribu kuonyesha ni kiasi gani nchi hii hata kwa kutumia mfano huu wa kipindi tu cha uongozi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni mambo gani tumeyafanya na kwa kiwango gani. Nashukuru sana kwani wako Wabunge ambao wamekiri kwamba kazi iliyofanyika ni nzuri. Lakini wapo bado wenzangu wanaosema yote haya ni lelemama tu!

 
 

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana baadhi ya wachangiaji hapa wametukumbusha wimbo wa “Mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe”. Wengine wakasema; “Wana macho lakini hawaoni, na wana masikio lakini hawasikii”. 

 
 

Mheshimiwa Spika, lakini niseme vilevile kwa kuwambusha tu iko ile hadithi moja ambayo wengi tunaijua ya Sungura Mjanja, kashindwa kupata ndizi zilizoiva, aliposhindwa akasema: Ah! kwanza hazikuiva akaondoka anasononeka, anatukana, analaani lakini ukweli ukabaki palepale kwamba, ni kwa sababu ameshindwa kuzifikia zile ndizi.

 
 

Mheshimiwa Spika, wakati wa Uhuru tulikuwa na Chuo Kikuu kimoja tu, leo tuna vyuo 32, tena kana kwamba haitoshi, Bunge lako hili liko pua na mdomo na Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu ambacho sasa hivi kimeishadahili wanafunzi zaidi ya 10,000, Chuo Kikuu kikubwa kuliko vyote hapa nchini. Wote wanaokwenda kutembelea pale hawaamini kwamba, ni nchi yetu imefanya haya, hawaamini zaidi kwamba hili limefanywa na Serikali kwa kutumia vyanzo vyake. Lakini bado watu wanasema yote haya si chochote. Ah! Basi tutamuachia Mungu.

 
 

Mheshimiwa Spika, ninatoa rai hii kwa Watanzania wenzangu nikiamini kabisa kwamba katika kuyasema haya nimejitahidi kusema bila kujali jinsia, itikadi zetu za kisiasa, imani zetu za dini. Nimejaribu kuonesha tu kwamba, kama yapo mazuri ambayo yamefanywa na mwenzenu mmoja ni vyema kwa ungwana tukaamua kumpongeza huyo.

 
 

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya ya utangulizi naomba sasa uniruhusu nipitie baadhi ya maeneo ambayo nadhani ni vizuri nikayasema.

 
 

KILIMO

 
 

Mheshimiwa Spika, eneo moja lililopata michango mingi ni la kilimo. Wako waliotushauri vizuri sana na ushauri wao ninataka nikuhakikishie Mheshimiwa Spika, tutauzingatia.

 
 

Mheshimiwa Spika, lakini wako vilevile mmoja mmoja waliyoyasema ambayo siyo mazuri sana, mengine kwa kubeza. Lakini ninataka nikuhakikishie kwamba Serikali imedhamiria kwa kuleta mapinduzi ya kweli ya kilimo kwa maana ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara, mifugo, uvuvi na raslimali zinazotokana na misitu.  

 
 

Mheshimiwa Spika, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tumeona tuyape kipaumbele maeneo haya kwa kuwa Watanzania wengi ndiko wanakotegemea. Nakubali kwamba katika bajeti hii Kilimo kimepewa kipaumbele cha Nne. Lakini naomba vilevile niseme kwamba, hivi ni nani asiyeona kwamba, pamoja na kufanya kilimo kuwa kipaumbele yako mambo mengi ambayo tumeyataja yatakayosaidia sana katika kuongeza ufanisi wa kilimo.

 
 

Moja ni ongezeko la bajeti, lakini pili ni juhudi ambazo tumezifanya kupunguza baadhi ya kodi pamoja na maeneo mengine ili kuvutia uwekezaji katika eneo hili.

 
 

Mheshimiwa Spika, lakini pili ni kwamba, kwa hapa tulipofika kwanini mtu uone tatizo kuwa na bajeti ambayo kipaumbele chake ni katika elimu? Tumefanya makubwa, tunahitaji kuyaimarisha na Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, asubuhi ametoa ufafanuzi mzuri sana. Lazima haya mafanikio tuliyoyapata sasa tuyaimarishe, tuhakikishe tunajenga sasa nyumba za walimu, tuhakikishe tunajenga maabara nyingi, na tuhakikishe vilevile sasa kwamba miondombinu ya msingi sasa inakamilika na kuimarishwa vizuri.

 
 

Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ya Awamu ya Nne si kukibeza kilimo, ni kutaka itambulike tu kwamba, pamoja na yote yanayosemwa dhamira ya Serikali iko palepale na tuna hakika tutafanikiwa.

 
 

Mheshimiwa Spika, pamoja na hali hii bado nina amini kwamba wote sasa tunafahamu kwamba, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika eneo hili la kilimo azma yake kupitia Kilimo kwanza ni dhahiri, na mimi nataka niseme uamuzi huu ni wa dhati kabisa na tumedhamiria kushirikisha sekta binafsi kwa nguvu sana pamoja na taasisi nyingine za fedha na wadau wengine ili kuweza kuongeza uwezo wa sekta hii katika kuchangia katika Pato la Taifa na mimi ninaamini tutafika huko.

 
 

UTEKELEZAJI WA KILIMO KWANZA

 
 

Mheshimiwa Spika, tangu uamuzi wa kutekeleza azma hii yapo mambo mengi yamefanyika. Hata hivyo, ipo hoja kwamba utekelezaji wa Kilimo Kwanza haujapewa kipaumbele kwa maana ya kuwepo mabwana shamba, mbolea, mbegu bora za kisasa na uratibu maalum wa mikoa yote. Aidha tunahitaji uhakiki wa miundombinu, masoko na bei nzuri.

 
 

Mheshimiwa Spika, tunakubali na tunayafanyia kazi chini ya uongozi wa kiongozi thabiti kabisa Mzee wangu Stephen M. Wasira, haya yote ni baadhi ya maeneo ambayo tumeyapa kipaumbele kikubwa sana. Ndiyo maana tumeamua kutoa ruzuku ya mbolea, madawa na mbegu bora, tumeamua kuongeza idadi ya wagani na bajeti ya umwagiliaji, tumeamua ununuzi wa zana za kilimo upewe kipaumbele, tumeamua kuanzisha benki ya kilimo kwa madhumuni hayo hayo.

 

 

 

Vilevile Wizara, Mikoa na Wilaya zimeagizwa kuweka mipango ya utekelezaji na tayari mipango ipo kwenye mipango ya mwaka 2010/2011. Vilevile Sekta Binafsi kama nilivyosema sasa imehamasishwa ili ishiriki kikamilifu katika eneo hili.

 

 

 

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2010/2011 sekta ya kilimo imepewa kipaumbele na hivyo kupewa vivutio vifuatavyo;

 
 

o   Msamaha wa kodi katika usafirishaji wa bidhaa za kilimo, ikiwa ni pamoja na miwa, katani na chai.

 

 

 

o   Msamaha wa kodi kwa mashine za zana za kukusanyia mazao ya maziwa.

 

 

 

o   Msamaha wa kodi, VAT kwenye zana za kilimo ikiwa ni pamoja na combine harvesters, hay making machines na mowers.

 

 

 

o   Ushuru wa asilimia sifuri (Zero Rated VAT) kwa mafuta ya kupikia yanayozalishwa humu nchini.

 

 

 

o   Msamaha wa kodi kwa vifungashio vya juisi na mazao ya maziwa

 

 

 

o   Kutoza ushuru wa mazao kati ya 3% -5% kwa vyakula vya mifugo na mashudu.

 

 

 

o   Msamaha maalum wa vifaa vya mifugo na madaktari wa mifugo.

 
 

Mheshimiwa Spika, yote haya ni katika kuonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Nne katika eneo hili.

 
 

Mheshimiwa Spika, yapo malalamiko vilevile kuhusu power tillers. Mheshimiwa Waziri alilieleza vizuri sana asubuhi hii na mimi ninataka tu niongeze kwamba, wakati mwingine tofauti zinatokana na wapi matrekta hayo yametoka. Mengine yanatoka China, mengine yanatoka Japan, yako yanayotoka India, kwa hiyo, hii zote ni namna ambazo zinasababisha gharama hizi ziweze kubadilika.

 
 

Mheshimiwa Spika, hata hivyo Serikali imekwishaliona hilo, tunalifanyia kazi na tunaamini kabisa tutaweza kusimamia vizuri zaidi ili bei za vifaa hivi zisiwe kubwa kuliko matarajio ya Watanzania. Nataka niwakumbushe kwamba, Tanzania inahitaji wastani wa matrekta 18,000; sasa hivi tunayo karibuni 9,500 tu. Tunaagiza wastani wa trekta 200 mpaka 300. Hivi sasa inakadiriwa kwamba tuna majembe ya kukokotwa na wanyama ‘plau’ 820,000, mikokoteni milioni 1.3 na inakadiriwa kwamba tuna majembe ya mkono takribani milioni 14. Hii ni dalili wazi kabisa kwamba ni lazima kasi katika eneo la kilimo iongezwe na tuweze kufanya vizuri zaidi katika miaka inayokuja.

 
 

MRADI WA MABASI YA WANAFUNZI NA MABASI YAENDAYO KASI

 
 

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nimejaribu kueleza juu ya programu mpya iliyobuniwa na benki yetu ya CRDB kuhusu utaratibu wa kusaidia kubeba wanafunzi pale mjini Dar es Salaam. Nataka nirudie nilichosema kuipongeza sana Benki hii kwa jambo hili zuri, na mimi nitalifanyiakazi kuhakikisha kwamba, suala la kodi linapewa nafasi ili liweze kutazamwa, ili liweze kuwa ni mchango mkubwa katika eneo hili, ili watu wengi zaidi katika sekta binafsi waone namna ya kuchangia katika eneo hili.  

 
 

Mheshimiwa Spika, lakini jambo hili halina budi kwenda sambamba na jitihada nyingine za kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam. Na moja ya mpango kabambe tulionao ni ule wa mabasi yaendayo kwa kasi. Sasa jambo hili limezungumzwa kwa muda mrefu lakini sasa nataka niwahakikishie Watanzania kwamba, jambo hili sasa karibu litakamilika na utaratibu wa kujenga utaanza. Tayari tumeishapokea Dola za Marekani milioni 122 baada ya kuweka saini mkataba. Lakini vilevile nataka niwaarifu Watanzania kwamba, barabara tunazotarajia kuzijenga zina urefu wa kilomita 20.9 ikiwa ni upanuzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni, na barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi Morocco katika hatua ya kwanza. Barabara nyingine zitafuata baada ya hapo.

 
 

Mheshimiwa Spika, katika hatua hii vilevile tutafanya ujenzi wa vituo vya stesheni za mabasi (bus stations) vitano. Vituo vikubwa 29 na vituo vidogo 6 na karakana 2 za kuegesha mabasi (depots) na kwa sasa tayari tumeishatiliana saini mkataba kwa ajili ya kuanza kuhamisha nguzo za umeme za TANESCO ambao uliwekwa tarehe 31 Mei, 2010 na Mkandarasi anaendelea na hilo zoezi. Pia Jumatatu, tarehe 21 Juni 2010, tutawekeana saini kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha Kivukoni na mkataba wa ujenzi wa vituo vingine 29. Ni matumaini yangu kwamba, mpango huu utakapokamilika utasaidia sana kupunguza kero hii jijini Dar es Salaam na utasaidia vilevile katika ubebaji wa wanafunzi.

 
 

UDHIBITI WA FEDHA ZA SERIKALI

 
 

Mheshimiwa Spika, eneo jingine ambalo limesemwa na Wabunge wengi na mkazo mkubwa ambalo namimi nakubaliana nao ni udhibiti wa fedha za Serikali. Nakubaliana kabisa na Wabunge wote waliosema jambo hili.Yapo mawazo kwamba Serikali ipunguze safari za nje kwa watumishi wake na kuzingatia tu zenye tija ili kupunguza gharama za uendeshaji na badala yake zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

 
 

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunahitaji kutafuta utaratibu wa kudumu katika kudhibiti matumizi. Kwa sasa Serikali inao utaratibu maalum wa kutoa vibali kwa safari za nje. Aidha, vibali maalum hutolewa kwa safari muhimu zenye manufaa kwa nchi. Serikali itaendeleza juhudi hizo na kuhakikisha tunabana zaidi ili tuweze kuokoa fedha zisizokuwa lazima kutumika huko. Vilevile mmetoa maoni kuhusu hali ya udanganyifu, ubadhirifu wa matumizi yasiyo mazuri ya raslimali. Baadhi ya udanganyifu huu unatokana na majengo yasiyofuata ramani na ubora na mambo haya sasa tunayafanyiakazi. Serikali muda wote imekuwa ikisimamia na kudhibiti matumizi mabaya ya raslimali zake. Aidha, imeanzisha Kitengo cha Kufuatilia Matumizi kwenye Miradi ya Serikali ambacho kiko Hazina, na pia kuna Kitengo cha Wataalam wa Kukagua Miradi ya Ujenzi.

 
 

Mheshimiwa Spika, Serikali pia kwa kushirikiana na Bodi ya Wakandarasi imeendelea kuimarisha udhibiti wa ujenzi wa majengo mbalimbali ili yazingatie viwango, ubora, ramani na mipango miji na thamani ya fedha. Tutaendeleza juhudi hizi.

 

 

Mheshimiwa Spika, nataka nichukue nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge, viongozi na wanachi kuendelea kuisadia Serikali kufichua matumizi mabaya ya fedha.

 
 

MATUMIZI YA FEDHA KATIKA SERIKALI MITAA

 
 

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwa msisitizo mkubwa juu ya eneo ambalo vilevile limesemwa kwa nguvu sana ambalo linalohusu kwa ujumla Serikali za Mitaa. Hili ni eneo ambalo bado tunahitaji kulifanyiakazi kwa nguvu sana. Serikali imefanyakazi kubwa kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha katika maeneo ya Serikali za Mitaa: Vijijini, kwenye Kata na kwenye Wilaya. Lakini bado tunahitaji kudhibiti kikamilifu hatua zote zinazoweza kuwa ni mianya ya kuweza kufanya fedha hizo ziibwe au zitumike isivyotakiwa.

 
 

Mheshimiwa Spika, Serikali imejitahidi, tumeweza kuwajengea uwezo Serikali za Mitaa kwa kiasi kikubwa. Tumefanya hivyo kupitia Capital Development Grant, pamoja na Capacity Building Grant. Lakini pamoja na mambo yote haya tuliyofanya, Wizara vilevile kwa namna zake zimejaribu kusaidia Halmashauri kwa kuzijengea uwezo.

 
 

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni Wizara ya Kilimo kupitia ASDP, Wizara ya Maji kupitia Rural Water Sewage and Sanitation Program (mradi wa maji safi na maji taka), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kupitia Mpango wake wa utoaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia kujenga uwezo, na Wizara ya Elimu na Ufundi kupitia mpango wake wa kutoa msaada au fedha kwa ajili ya kujenga uwezo.

 
 

Mheshimiwa Spika, kiasi cha fedha ambacho mpaka sasa kimeishatolewa ni shilingi bilioni 26, kati ya hizo shilingi bilioni 18 zimeishatumika na kiasi kingine bado. Kwa hiyo, ni jitihada kubwa, kutokana na jitihada hizi tumeweza kutoa mafunzo kwa Madiwani pamoja Watumishi 77,030 ili kuwajengea uwezo ili waweze kufanya vizuri zaidi katika kusimamia fedha za umma.

 
 

Mheshimiwa Spika, tathmini ya ukaguzi ya mwaka 2009/2010 imeonesha asilimia 80.3 ya Halmashauri zilizopimwa zimekutwa zikiwa na watumishi wenye sifa na uwezo unaotakiwa. Tatizo hapa ni sisi lazima sasa tujipange vizuri kuweza kusimamia mianya yote ambayo inaweza kuwa bado inavujisha mali ya umma. Nataka nitoe wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, timizeni wajibu wenu, jitahidini kuwa karibu sana na hizi Halmashauri. Msiogope, wakati mwingine mnaogopa kupita kiasi mnashindwa hata kuweza kuhoji mambo ambayo ni halali kabisa. Hakuna atakayekufanyia lolote endapo katika kutekeleza majukumu yako unachotaka kufanya ni kunusuru fedha za umma.  

 
 

Ziko dalili zimeanza kujitokeza za kupungua kwa Halmashauri zinazopata hati chafu za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Pamoja na hayo bado tunayo kazi kubwa ya kuwa na uhakika kama fedha hizo zilizotoa hati safi ni kweli zinawiana na miradi au utekelezaji wa miradi ambayo iko katika maeneo hayo, yaani thamani ya fedha zetu. Kwa hiyo, bado tuna changamoto nyingi na tutajitahidi kuweza kuendelea kufanya kila litakalowezekana kuhakikisha kwamba tunasimamia vizuri eneo hili

 
 

Mheshimiwa Spika, tayari katika kipindi cha mwaka 2005 mpaka 2010 Watumishi 1556 katika katika Halmashauri walichukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kutokana na kukiuka kanuni, taratibu na Sheria za Utumishi wa umma. Kati ya hawa watumishi 1063 katika halmashauri hizo walifikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria, wengine baadhi yao ni Wakurugenzi wa Halmashauri zenyewe na maeneo ambayo hasa yalisababisha kufikishwa kwao mahakamani ni yaleyale mnayosema Waheshimiwa Wabunge, matumizi mabaya ya fedha, upokeaji wa rushwa, kuhujumu uchumi, wizi wa mali ya umma na wakati mwingine kughushi.

 
 

Idadi ya watumishi waliohamishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa sababu ya kutaka kuimarisha utendaji kazi katika maeneo mbalimbali kwa kipindi hicho ni 2,858. Wote hawa lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu hawakai katika eneo moja kwa muda mrefu na kujenga mazoea na kufanya kazi kwa mazoea.

 

 

UVUNAJI HARAMU WA MISITU YA SHENGENA

 
 

Mheshimiwa Spika, imetokea hoja hapa nzuri ya uvunaji haramu wa misitu katika Misitu ya Shengena. Nimeona hili nilieleze kwa sababu ni jambo kubwa na linagusa eneo muhimu sana la hifadhi ya mazingira ambalo linawiana vizuri sana na mabadiliko ya tabianchi.

 
 

Mheshimiwa Spika, taarifa ya uvunaji haramu wa misitu katika eneo la msitu wa Shengena, msitu ambao uko katika Hifadhi ya Mkomazi, ilitolewa na Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki. Kulingana na taarifa hiyo uvunaji huo unafanywa na majangili ambao pamoja na kutokufuata taratibu watu hao hawana vibali vinavyowaruhusu kuvuna katika misitu katika eneo hilo.

 
 

Aidha, majangili hao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi mbalimbali kuwa wamewatuma kuja kufanya uvunaji katika eneo hilo kitendo ambacho si cha kweli. Waongo, uongo mtupu! Pia majangiri hao wamekuwa wakikata miti hovyo kwa njia batili na wakati mwingine kuchoma moto misitu.

 

 

Mheshimiwa Spika, uvamizi wa misitu huo ulikuwa kati ya mwaka 2005 na 2009 kwa ajili ya kuchimba dhahabu na bauxite. Uharibifu ulikuwa katika vyanzo vya maji, pia ukataji miti katika misitu. Taarifa zilizopo ni kwamba hali ya sasa ni shwari zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni na imedhibitiwa kwa ushirikiano kati ya Wilaya na Wizara ya Nishati na Madini. Hata hivyo, bado wapo wachimbaji wamejiingiza katika maeneo hayo na kuanza kuchimba na hivyo kusababisha makusudi mengine ya vijana kuvamia tena eneo hili. Tutaendelea kufanya juhudi zaidi ili kuhakikisha tunadhibiti uharibifu huo usiendelee.

 
 

Mheshimiwa Spika, eneo jingine ambalo limezungumzwa hapa na Waheshimiwa Wabunge ni namna Serikali inavyokabiliana na tatizo la rushwa nchini. Suala hili ni vizuri tukarudi nyuma na kutazama tulipotazama hasa kwa lengo la kuangalia juhudi tulizofanya. Mwaka 2006 ndipo Serikali ilipounda Tume ya Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, ili kutazama eneo hili kwa upana na kutoa mapendekezo namna ya kuziba mianya katika maeneo mbalimbali. Tunaendelea kumshukuru sana Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba. Alifanyakazi nzuri ambayo imetupa namna nzuri zaidi na kubwa zaidi ya kujaribu kuendelea kupigana vita dhidi ya rushwa.

 
 

Mheshimiwa Spika, vita hii itaendelea, na ni vita yetu sisi wote. Nataka niwashukuru Wabunge kwa namna moja au nyingine kwani nanyi mmeendelea kusaidia sana katika kukemea na kukaripia sana tatizo hili la rushwa. Ninawashukuruni sana.  

 
 

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizo zote Serikali kwa upande wake imeweza kutunga Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004 yaani Public Procurement Act ya mwaka 2004. Imetunga vilevile Sheria ya Kuzuia Fedha Haramu ya mwaka 2006 The Anti-Money Laundering ya mwaka 2006. Serikali imeweza vilevile kutunga Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa The Prevention and Combating of Corruption Act, ya mwaka 2007, imeweza vilevile kutunga Sheria ya Maadili ya Viongozi ya mwaka 1995 na kuifanyia marekebisho yaani The Public Leadership Code of Ethics Act 1995. Yote haya ni jitihada za Serikali kulenga kukabiliana na tatizo hili kubwa ambalo tusipoangalia linaweza lisituletee matunda mazuri sana.

 
 

AKAUNTI YA MADENI YA NJE

 
 

Mheshimiwa Spika, tumekuwa muda wote tunaendelea kueleza kwa kiasi tunachoweza juu ya nini kilifanyika kuhusu suala zima la akaunti ya madeni ya nje yaani The External Payment Areas Account (EPA) iliyotoka katika Benki Kuu ya Tanzania. Tunaendelea kulieleza Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali yetu itaendelea kusimamia eneo hili, na tayari watu 13 wameishafikishwa mahakamani na kesi nyingine bado zinaendelea. Tutakapokamilisha uchunguzi wake nazo tutazifikisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye vyombo vya kisheria.

 
 

Mheshimiwa Spika, juhudi hizi ni lazima wote tutambue kwamba ni zetu wote na lazima tuzivalie njuga kwa nguvu sana ili tuweze kupambana na tatizo hili kubwa.

 
 

UANZISHAJI WA MAENEO MAPYA

 
 

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo limesemwa kwa nguvu ni suala zima la uanzishaji wa maeneo mapya. Mheshimiwa Celina Kombani ametoa maelezo asubuhi kuhusiana na Vitongoji, Vijiji na Kata na baadaye akasema maeneo yaliyobaki kwa sehemu kubwa ni eneo la Mheshimiwa Rais. Sasa nimeona kuliko kuacha Bunge hili mnaendelea kuliulizia ulizia nimeona pengine ni vizuri nitoe maelezo kwa ufupi.

 
 

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais tarehe 14 Juni, 2010 tayari amekwisharidhia uanzishwaji wa maeneo mapya katika maeneo mbalimbali na naomba niseme alichosema. Kwanza, katika mapendekezo yaliyowasilishwa kwake amekubali mapendekezo yote kuhusu kugawa Tarafa mpya nitazitaja. Pili, amekubali vile vile mapendekezo yote ya kugawa Wilaya isipokuwa eneo moja tu la Wilaya ya Bagamoyo. Tatu, amekubali mapendekezo ya kuunda mikoa mipya mitatu ambayo nayo nitaieleza, na Nne, kwa upande wa mkoa wa Mpanda ambao ulikuwa umependekezwa nao kuundwa kutokana na ukubwa wake ameshauri tusubiri kwanza ili mashauriano yafanyike kati ya Mkoa wa Tabora na Mkoa wa Rukwa. Hilo nalo tutalifanya kwa lengo la kuhakikisha kwamba jambo hili linafanyika kwa nia njema na kwa nia nzuri.

 
 

Mikoa

 

 

Mheshimiwa Spika, mikoa hiyo ni ipi? Mkoa wa kwanza ni mkoa wa Njoluma, wale wanaotoka kwenye eneo hilo wanalijua. Njoluma ni Njombe, Ludewa na Makete. Ingawa Mheshimiwa Rais amesema kwa nini usiitwe tu mkoa wa Njombe? Mbona mnaanza majina mapya? Mkoa wa pili ni mkoa wa Geita, baadae Bungeni humu tutatoa maelezo ya kina kuonyesha mkoa huo ulivyoundwa. Mkoa wa tatu ni mkoa wa Simiu, nao Rais amekubali uanzishwe na baadaye tutatoa kwa maandishi kueleza kwa ufafanuzi zaidi. Shinyanga ndiyo imeanzisha mkoa mwingine unaitwa Simiyu. Watu wa Geita mnaelewa kuna sehemu inayounganisha Kagera, Mwanza na Shinyanga inatumia jina hilo.

 
 

Wilaya

 
 

Mheshimiwa Spika, Wilaya mpya zitakazoanzisha wale wanaotoka kwenye maeneo hayo wanajua Wilaya ya Mulele, hii ni Wilaya ya Mpanda, Wilaya ya Gairo, Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Wilaya ya Kakonko, Wilaya ya Uvinza, Wilaya ya Nyasa, Wilaya ya Kaliua, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Butiama, Wilaya ya Buhigwe, Wilaya ya Ikungi, Wilaya ya Momba, Wilaya ya Wanging’ombe, Wilaya ya Nyangw’ale, Wilaya ya Mbogwe, Wilaya ya Itilima, Wilaya ya Mkarama, Wilaya ya Ushetu. Wanaojijua ndiyo maana unasikia wanapiga makofi maana wanajua hata Ushetu ni wapi.

 

 

Tarafa

 

 

Mheshimiwa Spika, Tarafa mpya alizoridhia zianzishwe ni Tarafa ya Tunduma, Tarafa ya Itaka, Tarafa ya Kizengi, Tarafa ya Nyaronga, Tarafa ya Kifura, Tarafa ya Mpwayungu, Tarafa ya Mima, Tarafa ya Nkoswe, Tarafa ya Ruaha, Tarafa ya Ngohelanga, Tarafa ya Hagati, Tarafa ya Bukombe, Tarafa ya Ushirombo, Tarafa ya Kasharunga, Tarafa ya Mkwedu, Tarafa ya Mkunya, Tarafa ya Mangaka, Tarafa ya Chalinze, Tarafa ya Minsukumilo, Tarafa ya Mamba, Tarafa ya Ndurumo na Tarafa ya Kindoroko. 

 
 

Mheshimiwa Spika, amekubali vile vile Tarafa zitakazotokana na kupandishwa hadhi baadhi ya Kata ambazo zimeshapandishwa hadhi ni Tarafa ya Kigonsera pamoja na tarafa ya Mkumbi. Iko vile vile Tarafa itakayotokana na marekebisho ya tangazo la Serikali ambayo katika tangazo la mara ya mwisho iliachwa ni tarafa ya Siha Kaskazini na yenyewe sasa itakuwemo katika tarafa hizo.  

 
 

Halmashauri

 
 

Mheshimiwa Spika, ziko Halmashauri vile vile ambazo zimeridhiwa nazo zianzishwe. Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mtaona zinaendana pamoja na Wilaya hizo mpya. Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Halmashauri ya Wilaya ya Mulele, Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Halmashauri ya Wilaya ya Kwela, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Halmashauri ya Wilaya ya Mkarama, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.

 
 

Nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Halmashauri ya Mji wa Kahama, Halmashauri ya Mji wa Masasi, Halmashauri ya Mji wa Handeni, Halmashauri ya Mji Nzega, Halmashauri ya Mji wa Lindi imepandishwa hadhi kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kama alivyosema Mheshimiwa Kombani asubuhi hii. Bado tutadaiwa eneo moja ambalo nalo itabidi baadae tuje tulieleze ni Halmashauri ya Jiji la Arusha, bado tunakamilisha taratibu zake baada ya muda mfupi na lenyewe litatangazwa kulingana na hadhi yake.

 
 

UWEKEZAJI KATIKA MIRADI

 
 

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo nimeona nalo niligusie kidogo kabla ya kumalizia ni lile ambalo Mheshimiwa Ngasongwa amelizungumza alipokuwa anatoa mchango wake. Kwamba haitoshi tu kwa Serikali kujitapa kwamba tumekuwa na wawekezaji wengi, tuna miradi mingi hapa nchini imeanzishwa kama hatuwezi kujua ni kiasi gani cha miradi hiyo kweli imeanza kufanya kazi. Kwa hiyo kutokana na uhakiki uliofanyika miradi ambayo inatekelezwa kwa uhakika kwa sasa ni asilimia 80 na miradi 20 imekwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ukosefu wa mitaji, ucheleweshaji wa upatikanaji wa vibali kama vya ujenzi (building permit) na hati za kumiliki ardhi. Zoezi hili tunaendelea nalo chini ya Mamlaka ya Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).

 
 

Sambamba na hilo, kituo hiki cha TIC kimeanzisha Kitengo Maalum After Care Unit ambacho moja ya shughuli zake kubwa sasa ni kutembelea miradi iliyosajiliwa na Kituo hicho na kuona ufanisi wake kulingana na makubaliano tuliyofikia. Aidha, Serikali imejitahidi kuimarisha Kituo kwa kuitengea bajeti ya kutosha. Pia Kituo cha Uwekezaji sasa kinashirikiana na Mashirika ya Kimataifa kama vile UNIDO, UNTAD, WIPER pamoja na programu ya BEST inayochangiwa na wahisani mbalimbali. Aidha, Serikali imekwishateua Bodi mpya, Bodi mahiri ambayo tunaamini kwa kushirikiana na TIC na watendaji wake itaweza sasa kutuongoza vizuri na kutupeleka mahali pazuri.

 
 

MFUMUKO WA BEI

 
 

Mheshimiwa Spika, liko eneo moja ambalo nilidhani vile vile ni vizuri nikalisemea kidogo nalo lilisemwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kujaribu kuonyesha kwamba mfumuko wa bei unaoelezwa inawezekana si mfumko wa kweli kweli wa dhati inawezekana pengine ni maneno maneno tu ya Serikali. Kwa takwimu tulizonazo mwaka 2000 mfumko wa bei ulikuwa ni asilimia 6. Mwaka 2001 ulikuwa 5.1, mwaka 2002 ilikuwa 4.3, mwaka 2003 ulikuwa 5.3, mwaka 2004 ulikuwa 4.7, mwaka 2005 ulikuwa 5.0, mwaka 2006 ikapanda kuwa 7.3, mwaka 2007 ikawa 7, mwaka 2008 ikawa 10.3, mwaka 2009 ilikuwa 12.1 na hadi Aprili, 2010 ilikuwa 9.8, imeteremka kidogo kutokana na juhudi ambazo zimefanyika.

 
 

Serikali imekwishaeleza kwamba ziko sababu kubwa mbili kuu ambazo zinapelekea jambo hili kutokea. Moja ni ongezeko la bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa ujumla wake katika soko la dunia ambayo imekuwa ikipanda muda wote hata pale iliposhuka kidogo lakini haikutupa ahueni kubwa sana. Eneo la pili ni upungufu wa chakula hapa nchini ambao umesababisha bei kuwa kubwa na kwa hiyo kuongeza kwa kiasi kikubwa gharama hizo ambazo zinazaa mfumko wa bei.

 
 

Mheshimiwa Spika, pengine kwa kutoa mfano tu kwa upande wa mafuta nichukue petroli Januari, 2004 bei ya mafuta kwa tani moja ya petroli ilikuwa ni Dola 220.888. Mafuta ya taa na ndege ilikuwa ni Dola 304.64, dizeli ilikuwa ni Dola 271.35. Mafuta hayo hayo ilipofika Aprili, 2010 mwaka huu bei ya mafuta hayo kwa upande wa petroli ilikuwa ni Dola 778.62. Na kwa upande wa mafuta ya ndege na ya taa ilikuwa ni Dola 733.62. na kwa upande wa mafuta ya dizeli ilikuwa ni Dola 695.17.

 
 

Mheshimiwa Spika, hali hii inajitokeza vile vile katika hali halisi ya bei hizo hapa nchini. Januari, 2004 lita moja ya Petroli hapa nchini ilikuwa ni shilingi 725/-, mafuta ya taa ilikuwa shilingi 520/-, na dizeli ilikuwa shilingi 660/-. Mafuta hayohayo, Mei 2010 petroli ilikuwa ni shilingi 1,727.87, mafuta ya taa shilingi 1,225.70, mafuta ya dizeli ni shilingi 1,728.08. Ninachotaka kusema hapa ni nini? Ni kwamba, maelezo haya ya Serikali siyo tu yanasemwa kwa kujaribu kudanganya jamii au kutokutaka kutoa picha ya kweli. Ni kweli kwamba uko uwiano wa karibu sana kati ya gharama za mafuta ambazo ndio tunatumia kwa kiasi kikubwa katika bei za ulimwenguni na namna zinavyoathiri bei hizo hapa nchini. Tutaendeleza juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba tunadhibiti hali yoyote ile ambayo inaweza ikatumika na wafanyabiashara kufanya bei hiyo iongezeke wakati si lazima iongezeke. 

 

 

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chakula. Kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kipindi chote tangu mwaka 2005 Serikali imesimamia eneo la sekta hii vizuri sana na tumeweza kuzalisha chakula cha kujitosheleza kwa mwaka 2004/2005 kwa asilimia 103, mwaka 2006 kwa kiwango cha asilimia 102, mwaka 2006/2007 kwa asilimia 112, mwaka 2007/2008 kwa asilimia 106, mwaka 2008/2009 kwa asilimia 105, mwaka huu tunaamini tutakwenda zaidi ya asilimia 100. Kwa nini nalisema hilo? Nalisema hili kwa lengo la kuonyesha kwamba ziko juhudi za kweli ambazo zikiwekwa na Serikali na Watanzania wote eneo hili ambalo linachangia vile vile katika kuongeza mfumuko wa bei. Tunaweza kabisa tukashusha mfumko huo kwa kuwa na chakula cha kutosha ambayo bei yake ikiwa ndogo mfumko wa bei nao utashuka. Tatizo tulilonalo ni kwamba kwa sehemu kubwa chakula hiki kinatoka katika mikoa michache na inalazimika kulisha mikoa mingine ambayo ina ukame mkubwa. Hata hivyo Serikali itaendelea kufanya kila litakalowezekana ili tuweze kuhakikisha kwamba kazi hiyo inazaa matunda mazuri.

 

 

MAAFA

 

 

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie basi, liko jambo moja nalo limejitokeza kwa nguvu sana linalotokana na maafa yaliyotokea hapa nchini. Niliyaeleza wakati natoa maelezo wakati fulani, lakini naomba nilirudie leo. Yako maafa ya aina nyingi, lakini kwa safari hii nimesema Serikali itaangalia kwa dhati na kwa karibu sana suala zima la yale maeneo yaliyopata ukame katika maeneo ya ufugaji. Wilaya zote mikoa ya Arusha, Simanjiro na maeneo mengine Serikali imeshaanza kujaribu kutazama nini tufanye hata kama kitakuwa ni kidogo lakini kwa lengo la kuwaonyesha Watanzania kwamba tunatambua tatizo hili na Serikali iko tayari kujaribu kusaidia kwa kadri itakavyowezekana kuleta kitu ambacho kinaweza kikawatia moyo kidogo. Waswahili wanasema, “Kutoa ni moyo na wala sio utajiri”. Tutawaomba basi wananchi wa maeneo hayo yote washirikiane na Serikali tutakapokuwa tunaomba kupata maelezo ya ukweli ya dhati, takwimu za kweli juu ya kiwango cha athari, idadi ya wanyama waliokufa, familia zilizoathirika kikweli kweli kwa kiwango kikubwa na hawana namna nyingine yoyote ya kuweza kujisaidia.

 
 

La pili, Serikali vile vile imekubali kwamba kwa kuwa maafa haya kwa maeneo ya wafugaji si kwamba imewapunguzia wao wenyewe chanzo muhimu kwa mapato yao na chakula lakini vile vile kimeathiri sana uwezo wao wa kuweza kuchangia katika huduma za msingi. Ni wachangiaji wazuri sana katika ujenzi wa shule za sekondari, vituo vya afya na zahanati, lakini kutokana na hali hii sasa uwezo huo sasa umepunguka kwa kiasi kikubwa sana. Serikali imesema tutaliangalia angalau tuweze kuchangia katika kuwezesha hiyo miundombinu isibaki kama ilivyo ili kuwezesha watoto waweze kwenda shule na vituo vya afya kujengwa. 

 
 

Mheshimiwa Spika, ziko aina nyingine za maafa ambazo nilizieleza wakati natoa maelezo yangu lakini Prof. Sarungi naye amekuja na maafa ya aina yake. Katika mapigano yaliyotokea kule Rorya kati ya koo na makabila mbalimbali, ni kweli na yale ya mwisho kabisa ni mabaya ni yale yaliyosababisha vifo vya watu 40 na ng’ombe wengi kuibiwa na kuchomwa nyumba nyingi. Ametoa rai kwa Serikali, kwamba Serikali ingeangalia eneo hili waone kama ni namna gani tunaweza tukasaidia pengine kuona namna yoyote ile ya kuweza kuwapunguzia wale hasa ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa. Ni wazo kubwa, ni wazo jema na ni kweli yalitokea. Serikali inakubali kwamba italiangalia hasa kwa zile familia zilizochomewa nyumba ambao walipata matatizo makubwa namna ya kuishi katika maeneo yao.

 
 

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya naomba nirejee nilichosema kwamba nimejitahidi kuyapitia maeneo yale ambayo nimeona ni makubwa lakini ni kweli hata mimi sikuweza kuyamaliza yote. Tutajitahidi kujaribu kuyatolea maelezo ya kina kwa wakati muafaka ili kila Mbunge aweze kujua lile alilotolea mchango na lile ambalo aliweza kulisemea basi lipate maelezo ya kina na ufafanuzi stahiki kwa lengo la kuwezesha kujua ni nini Serikali imedhamiria kufanya katika eneo hilo.

 
 

HITIMISHO

 
 

Mheshimiwa Spika, narejea nikushukuru wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana Wenyeviti wako, niwashukuru sana Wabunge wenzangu ambao tumesaidiana kwa namna nzuri sana katika kipindi chote kuhakikisha kwamba Bunge hili linafanya kazi yake vizuri na kwa viwango vinavyotakiwa na mimi nimefarijika sana. Nataka vile vile nitumie nafasi hii kuwashukuru sana Mawaziri wenzangu na hasa Mawaziri wale ambao wanasaidia moja kwa moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa namna ya pekee ambayo wamefanya kazi na mimi kwa karibu sana katika kipindi chote wameshauriana nami kwa namna nzuri sana na hivyo kutuwezesha kuweza kutoa mchango wetu mdogo kwa kadri tulivyoweza.

 
 

Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya. Viongozi hawa mikoani na Wilayani ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya Watanzania. Nachelea na sikubaliani hata kidogo na baadhi ya Wabunge wachache ambao mara nyingine huwa wanasahau na wanafika mahali wanasema hawaoni sababu za Mkuu wa Wilaya kuwepo. Tumuondoe leo Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Spika siku mbili mtasema mrudisheni. Sababu zake ni dhahiri, haya mapungufu yote mnayoyaona katika Halmashauri zetu, katika Serikali zetu kama kusingekuwa hata na juhudi ndogo za Wakuu wa Wilaya hali ingekuwa mbaya sana. Nataka niwasihi sana Waheshimiwa Wabunge tuendelee kuthamini kada hii ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya pamoja na Maafisa Tarafa ambao wanaisaidia Serikali Kuu. Tuwasaidie wajenge uwezo zaidi, waweze kuwa ndio Maaskari wetu wa mbele, majemadari wa karibu kabisa katika kusimamia Serikali za Mitaa ambazo ndiyo vyombo vya utekelezaji ili waweze kutimiza majukumu yao vizuri zaidi.

 
 

Mheshimiwa Spika, nataka niwashukuru Madiwani wote nchi nzima, Wakurugenzi wao chini ya uongozi wa Wenyeviti wao na Mameya wao kwa namna ambayo pamoja na mambo yote yanayosemwa bado kuna Halmashauri zimeendelea kufanya vizuri, tuwaombe na wale wengine ambao bado hawajajipanga vizuri waige mifano kwa wenzao wanaofanya vizuri na wahimize zaidi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Mheshimiwa Waziri wa Sheria na Katiba alisema “Tatizo tulilonalo hapa wako watu wamezoea kupokea rushwa, wako watu wamezoea kuiba, wako watu wamezoea kusema uongo na kudanganya. Wakati mwingine kuweza kuwabaini watu wa namna hii inataka juhudi za pamoja. Serikali peke yake si rahisi kwa hiyo tunaomba sana Watanzania wote, Waheshimiwa Wabunge, viongozi wote, wote tudhamirie kwa dhati kutambua kwamba fedha zinazokwenda katika maeneo yetu ya vijijini ni fedha nyingi sana, zikisimamiwa vizuri zikafanya kazi iliyopangwa matokeo yake ni mazuri maradufu. Ni imani yangu kwamba katika vipindi vijavyo kuanzia mwaka huu wa fedha tunaomalizia tutaweza kufanya vizuri zaidi kwa kadri itakavyowezekana.

 
 

Mheshimiwa Spika, nirejee sasa kuwashukuru wapigakura kutoka Jimbo la Mpanda Mashariki wamenipa heshima kubwa, upendo mkubwa sana kwa kipindi chote. Ninawashukuru. Sana viongozi wangu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda kwa kuendelea kunisaidia kunishauri na kila walipoweza kwenda kunisemea vizuri kwa Watanzania. Nawashukuru sana. Niwashukuru viongozi wa Rukwa kwa ujumla wao kwa namna ambavyo tumefanya kazi nao kwa pamoja.

 
 

Mheshimiwa Spika, najua kazi hizi zinakuwa ni nzito na ngumu sana. Niendelee kumshukuru Mama Tunu Pinda kwa kunivumilia sana.

 
 

Mheshimiwa Spika, mwisho naomba nimalizie kwa kumshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Rais huyu amefanya kazi kubwa, kazi inayoonekana mbele ya Watanzania. Mimi ninayo imani kubwa sana kwamba atashinda kwa kishindo.

 
 

Lakini pengine si vibaya nikamshukuru Mheshimiwa Shibuda ambaye baada ya jitihada zote alizofanya kama ilivyo kawaida yake, juzi alifika mahali akasema hapana anaahirisha nia yake na dhamira yake ya kutaka kugombea nafasi hii kupitia Chama cha Mapinduzi. Hakusema ameahirisha kwa kipindi gani lakini tunaomba tumtakie mema kwenye Jimbo lake Mungu amjalie kufanya kazi vizuri kwa kadri atakavyoweza.

 

 

Mheshimiwa Spika, imani yangu ni kwamba Wabunge wengi tutarudi hapa ndani, ninawatakia kila la kheri mfanye kila litakalowezekana. Kwa hiyo ni vizuri tukubali kwamba kwa mfumo wa demokrasia tuliojiwekea anything is possible. Wanaotuchagua ni Watanzania. Wenye maamuzi juu yetu, ni Watanzania. Lets get prepared kwa lolote watakalokuwa wametuamulia.

 
 

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naomba sasa nitoe hoja.

 

 

 

 

 

Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd