Home | News | Pinda: Michezo irejeshwe shule zote na vyuo siyo sekondari tu
News
Speeches

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

Hotuba ya Mheshimiwa Mizengo P. Pinda (Mb) Waziri Mkuu Wakati wa Kufungua Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu vya Dodoma katika Ukumbi wa African Dreams – Dodoma, tarehe 25 Juni 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya katika sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu zilizofanyika kwenye Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Februari 9, 2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Pinda: Michezo irejeshwe shule zote na vyuo siyo sekondari tu

Pwani,20 June 2010

 
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema uamuzi wa kurejesha michezo mashuleni siyo kwa shule za Sekondari tu bali kuanzia za msingi hadi Vyuo vya Elimu ya Juu.
 
Alikuwa akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye Kituo cha Elimu cha Kibaha, mjini Kibaha, mkoani Pwani leo (Jumapili, Juni 20, 2010).
 
“Maelekezo ya Rais Kikwete ya kurejesha michezo mashuleni ni kwa shule zote na vyuo, ili kuendeleza vipaji vya vijana katika  michezo na elimu nchini,” alisema.
 
Waziri Mkuu pia alielekeza kuwa michezo hiyo iwashirikishe pia wanafunzi wenye ulemavu wa viungo kwa kuwa nao wanaihitaji na wanaweza kucheza michezo mbalimbali.
 
Alitaka pia shule zote ziwe na viwanja vya michezo na kwamba Halmashauri za Miji, Manispaa na Vijiji zihakikishe kuwa maeneo yaliyotengwa kwa michezo yanatumika kwa shughuli hiyo tu na yanatunzwa na kuendelezwa.
 
Mhe. Pinda aliyashukuru makampuni yaliyochangia vifaa kwa UMISSETA na kuyataka mengi yafanye hivyo kwa kuwa yatakuwa yanatimiza wajibu wao wa kuisaidia jamii (corporate responsibility).
 
Kanda 12 za mikoa mbalimbali nchini zinashiriki katika michezo hiyo, ikiwa ni pamoja na kanda moja ya mikoa mitano iliyoko Unguja na Pemba.
 
Michezo inayoshindaniwa ni Mpira wa Miguu kwa wanaume na wanawake, Mpira wa Mikono, Mpira wa Meza, Mpira wa Kikapu na Riadha.
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe alisema kwa sasa michezo imerejeshwa shuleni kwa kuanzia na Sekondari, lakini baadaye itarejea kote.
 
Michezo mashuleni ilikuwepo tangu zamani lakini katika miongo ya hivi karibuni iliondolewa na baadaye zikatolewa lawama  kuwa kuondolewa huko ndiyo chimbuko la kudorora kwa vipaji vya michezo nchini.
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd