Home | News | Sekta binafsi kushirikishwa zaidi katika uwekezaji - Pinda
News
Speeches

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

Hotuba ya Mheshimiwa Mizengo P. Pinda (Mb) Waziri Mkuu Wakati wa Kufungua Kongamano la Vijana wa Vyuo Vikuu vya Dodoma katika Ukumbi wa African Dreams – Dodoma, tarehe 25 Juni 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji Getrude Nyaulawa ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Kawe jijini Dar es salaam November 11,2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Sekta binafsi kushirikishwa zaidi katika uwekezaji - Pinda

Dodoma,19 June 2010

  
SERIKALI inatarajia kuwasilisha Bungeni muswada wa sheria ya kuratibu ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuendeleza uwekezaji wa kiuchumi nchini.
 
Hayo yalitangazwa na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), kwenye hoteli ya New Dodoma leo (Jumamosi, Juni 19, 2010).
 
Mhe. Pinda alisema maara baada ya Sheria hiyo kupita, kinatarajiwa kuundwa kitengo maalum cha uratibu huo kwenye kituo cha TIC ili kuendeleza dhana ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
 
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliitaka Bodi kuisimamia TIC ili Tanzania ifanye vizuri katika Urahisi wa Kufanya Biashara (ni ya 131 duniani); Kuondoa Kero katika Taratibu za Forodha (ya 119); Ugumu katika kuajiri (ya 124) na Kiwango cha Kuweka Akiba (ya 124)
 
“Tunapoangalia nafasi yetu duniani katika takwimu hizi tunapaswa kujiuliza kwamba, tumeteleza wapi ili tujisahihishe,” alisema.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Emmanuel Ole Naiko alisema kuwa Tanzania sasa iimeanza kuwajenga wawekezaji wa ndani.  
 
“Wawekezaji wa ndani ni muhimu sana kuwekewa mazingira mazuri kwani Tanzania ni kwao na jinsi wanavyopata nguvu ndivyo wanavyozidi kuwekeza,” alisema.
 
Alitoa mfano wa Mtanzania mzawa anayemiliki kampuni ya usafirishaji wa ndege ya Precision Air aliyeanza kwa kusafirisha abiria 67,000  mwaka 1988/1989 kwa kutumia ndege mbili ndogo.
 
“Kufikia mwaka huu wa 2009/2010, Precision Air uwekezaji wake umefikia Dola za Marekani milioni 200, wana ndege 11 za ngazi ya kati na kubwa za Boeing mbili na uwezo wa kusafirisha abiria 700,000,” alisema.
 
Katika shughuli hiyo, Wajumbe wa Bodi ya TIC, akiwemo Mwenyekiti wake, Balozi Elly Mtango, walikabidhiwa alama za utambulisho za TIC kwa ajili ya kuitangaza Tanzania.
 
Wajumbe wengine wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC ni mfanyabiashara binafsi, Bw. Salum Shamte; Mwanasheria wa kujitegemea, Dk. Hawa Sinare; Prof. Andrew Temu; Katibu Mkuu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bibi Maimuna Tarishi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bibi Joyce Mapunjo.
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd