Home | News | Waomba Mpwapwa TTC kiwe Chuo kishiriki cha UDOM
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya katika sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu zilizofanyika kwenye Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Februari 9, 2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Waomba Mpwapwa TTC kiwe Chuo kishiriki cha UDOM

Dodoma,7 February 2010

 
UONGOZI wa mkoa wa Dodoma umeiomba Serikali iangalie uwezekano wa kukipandisha hadhi Chuo cha Ualimu cha Mpwapwa ili kiwe Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kama njia ya kuharakisha kupunguza tatizo la uhaba wa walimu nchini.
 
Ombi hilo lilitolewa jana jioni (Jumamosi, Februari 6, 2010) mjini Mpwapwa wakati wa maadhimisho ya miaka 33 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa wilayani humo.
 
Akitoa salamu za chama hicho, Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma, Kapteni (Mst.) John Barongo alisema Chuo cha Ualimu Mpwapwa kimekuwepo nchini kwa muda mrefu na kina sifa ya kutoa mafunzo kwa walimu.
 
Alisema ili kuziba pengo la walimu waliobobea kwenye fani hiyo, wanaiomba Serikali ikipandishe hadhi chuo hicho ili kiwe chuo kishiriki cha UDOM.
 
Chuo cha Ualimu Mpwapwa ambacho kilianzishwa tangu mwaka 1892 chini ya utawala wa Mjerumani wakati huo kikiendeshwa mjini Tanga na kutoa mafunzo katika fani za elimu, kilimo, ufundi na maarifa ya nyumbani.
 
Mwaka 1920 kilihamishiwa Dar es Salaam wakati wa utawala wa Waingereza na mwaka 1925 kilihamishiwa Central Province na kujengwa Mpwapwa ambapo kipo hadi sasa.
 
Chuo hicho kina jumla ya wanachuo 1,452, ambao kati yao 688 ni wasichana na 767 ni wavulana. Pia kina watumishi 107 kati yao 57 wakiwa ni wakufunzi wenye shahada za uzamili (2), shahada za kwanza (39) na stashahada 16. Walimu wa shule ya mazoezi ni 29 na watumishi wasio wakufunzi ni 21.
 
 
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd