Home | News | Pinda amvua madaraka DED Bagamoyo na watendaji wake wakuu
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipongezwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu kwenye Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Februari 9, 2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Pinda amvua madaraka DED Bagamoyo na watendaji wake wakuu

Pwani,20 January 2010

 
 * Awateua wengine wapya watano kujaza nafasi zao
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewavua madaraka viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kutowajibika ipasavyo na kutozingatia kanuni za  fedha na kuwateua wengine wapya kujaza nafasi zao.
 
Waliovuliwa madaraka ni Mkurugenzi Mtendaji Bibi Rhoda Nsemwa; Mweka Hazina, Bw. Karol M. Wage; Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Bw. Naftal Rhemtullah; Ofisa Mipango, Bw. Aloyce Gabriel na Mkaguzi wa Ndani, Bw. Abdul Mwinyi.
 
Mhe. Pinda alitangaza uamuzi huo mjini Bagamoyo leo (Jumatano Januari 20, 2010) kwenye mkutano na viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, akiwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
 
Amewavua madaraka watendaji wakuu hao wa Halmashauri ya Wilaya kwa kutumia kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na kusema hatua nyingine za kinidhamu zitafuatia kadri itakavyoonekana inastahili.
 
Aliowateua kushika nafasi hizo ni Bw. Samuel Saiyanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Bw. Fidelis R. Nenetwa kuwa Mweka Hazina, akitokea Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
 
Wengine wapya Bagamoyo ni Fidelica Gabriel Myovelo, kuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa; Felista Chuki Masamba kuwa Mkaguzi wa Ndani akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na Prudence Mtiganzi kuwa Mhandisi wa Maji akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
                                                                                   
Alisema uamuzi wa kuwapumzsiha  watendaji wakuu hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo unatokana na mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Septemba na Oktoba mwaka jana.
 
Uchunguzi wa Mdhibiti unafuatia tuhuma za ukiukwaji wa kanuni za fedha, uzembe wa kufuatilia utekelezaji wa miradi na ubadhirifu Halmashauri hiyo.
  
Ripoti hiyo imebainisha ukiukwaji mkubwa wa kanuni za fedha, uzembe na kushindwa kuwajibika na matokeo yake kuzorota kwa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
 
Waziri Mkuu alisema kuwa pamoja na kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa Bagamoyo, Halmashauri nyingine nchini zikae chonjo na zitashughulikiwa kwa kuwa nazo zina matatizo yanayofanana na ya Bagamoyo.
 
Katika ziara yake ya siku moja ya Bagamoyo leo (Jumatano, Januari 20, 2010) Waziri Mkuu pia alikagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha miwa na mahindi unaoendeshwa na kampuni binafsi ya SEKAB.
 
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd