Home | News | China kutuma wataalamu wa Reli na Bandari
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea Taarifa kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG),Ludovic Utoh kuhusu mapato na makusanyo ya kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es salaam, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Julai 28, 2009. Mheshimiwa Pinda alimuagiza CAG kufanya uchunguzi huo baada ya kutembelea kituo hicho na kupata malalamiko kutoka kwa wadau Machi mwaka huu.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

China kutuma wataalamu wa Reli na Bandari

Dar es Salaam,15 January 2010

 
 
WAZIRI wa Biashara wa China, Bw. Chen Deming amesema Serikali yake itatuma timu ya waatalamu katika masuala ya biashara, reli na bandari kabla ya Juni mwaka huu ili waweze kukutana na wenzao wa Tanzania na Zambia na kuangalia jinsi ya kuimarisha sekta hizo.
 
Ametoa kauli leo (Ijumaa, Januari 15, 2010) wakati akizungumza na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam ambako alimweleza kwamba ziara yake inafuatia ahadi ambazo China ilizitoa kwenye Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia kuhusu Bara la Afrika uliofanyika mwaka 2009 mjini Sharm el Sheikh, Misri.
 
Alisema katika mkutano huo, nchi zilizoendelea ziliazimia kuzisaidia nchi zinazoendelea na katika zote China iliamua kuzisaidia nchi mbili tu kutoka Afrika ambazo ni Tanzania na Ethiopia. Pia alimtaarifu Waziri Mkuu masuala yaliyoafikiwa baina yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu.
 
“Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, tutatuma timu ya wahandisi wa reli (railway engineers) na bandari waje na wataalamu wa biashara ili wakae na wenzao wa Tanzania na Zambia na kubaini njia za kuikwamua reli na bandari … watafute njia za kuifufua ili iweze kuamsha viwanda vya uzalishaji kwenye maeneo ambako reli hiyo inapita,” alisema.
 
Alisema kufufuka kwa reli kutaimarisha siyo tu sekta ya usafirishaji mizigo na abiria bali pia kutaiinua sekta ya kilimo kwani mazao yanayozalishwa yatakuwa na uhakika wa kufikishwa kwenye masoko na hasa kama kutakuwa na viwanda vya usindikaji.
 
Waziri Deming alimweleza Waziri Mkuu kwamba wamekubaliana na Dk. Nagu na Waziri wa Viwanda, Maliasili na Utalii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bi. Samia Sululu Hassan kwamba Serikali yake itaangalia maeneo mapya ya kusaidia hasa katika suala la umeme wa jua na upepo.
 
Alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa maeneo ya zamani ya kusaidia utaalamu kwenye kilimo, tiba na afya yataendelea kupata misaada kutoka Serikali ya nchi hiyo.
 
Kwa upande wake, Waziri Mkuu alimshukuru Waziri huyo kwa uamuzi wa nchi hiyo kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya kilimo kwani inaonyesha kutambua jinsi Serikali ya Awamu ya Nne ilivyoazimia kuinua sekta ya kilimo.
 
“Tunaiomba Serikali yako itusaidie kuikuza Benki ya Kilimo Tanzania kama ambavyo niliona miaka ya nyuma wakati nilipozuru China kwamba kuna matawi ya benki ya kilimo kila mahali nilikopita… tusaidieni benki zote mbili, Benki ya Kilimo (TAB) na Benki ya Rasilimali (TIB) zinahitaji kuimarishwa katika hisa na uwezo wa kutoa mikopo kwa wakulima…,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
 
Alisema ana imani kuwa misaada hiyo itaisadia Tanzania kukua kiuchumi kwa haraka. “Kama China imeweza na imefanikiwa sioni ni kwa nini na sisi tusiweze…” alisema.
 
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkullo, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. George Mkuchika na maafisa wengine wa Serikali.
 
                               
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd