Home | News | Rais Kikwete aagiza JWTZ liende Kilosa, Dodoma
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipongezwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika sherehe za kumwapisha Waziri Mkuu kwenye Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Februari 9, 2008.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Rais Kikwete aagiza JWTZ liende Kilosa, Dodoma

Morogoro,9 January 2010

 
RAIS JAKAYA KIKWETE ameliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipeleke askari wake mara moja katika wilaya ya Kilosa ili kusaidiana na uongozi wa mkoa wa Morogoro na wa wilaya hiyo kukabili maafa yaliyowapata.
 
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa nyakati tofauti leo mchana (Jumamosi, Januari 9, 2010) wakati akizungumza na wakazi wa Mabwerebwere, Usagara na Kilosa Town wilayani Kilosa ambako kuna kambi za wahanga, mara baada ya kuzungukia eneo lililoathirika kwa kutumia helikopta ya polisi.
 
“Jana usiku nilizungumza na Mheshimiwa Rais na kumweleza taarifa ya mkoa ilivyobainisha ukubwa wa tatizo na jinsi nilivyowakuta wakazi wa kijiji cha Magomeni wakati nakuja huku... amewapa pole sana kwa maafa haya na akaniambia ameagiza JWTZ waje mara moja Kilosa na Dodoma kuja kuongeza nguvu kwa sababu ya uzoefu walionao katika kukabiliana na maafa,“ alisema Waziri Mkuu.
 
Kazi kubwa ya haraka watakayokuja kutusadia ni kuweka makazi ya muda kwa haraka zaidi ili mkipata mahali pa kukaa tuweze kuwatoa shuleni na watoto wetu waweze kuendelea na masomo kwani shule nyingi zinafungua Jumatatu ijayo (Januari 11,2010).
 
“Hili kwa Kilosa najua halitawezekana, itabidi nimuombe Waziri wa Elimu aruhusu baadhi ya shule zichelewe kufunguliwa wakati tukijipanga kuwapa makazi ya kuhamia... naamini wanajeshi watatusaidia hasa tukipata mahema zaidi,“ alisema.
 
Waziri Mkuu amesema baada ya kupita angani amebaini kuwa mto Mkondoa unatokea kwenye milima na unapoingia Kilosa unakuta uwanda mkubwa kwa hiyo unasambaza maji kwa haraka sana.
 
“Eneo linalokabiliwa na mafuriko ni kilometa za mraba 541.3, ukiwa angani unabaini kuwa ule mto hautambui tena njia yake... nyumba zimezingirwa na maji na nyingine zimepotea kabisa. Kuna kazi ya kuchimba sana ili kurudisha kina cha maji....,“ alisema.
 
Alisema hadi sasa watu 23,980 wameathirika na mafuriko haya na hizo ni sawa na kaya 5,605. Alisema nyumba 4,699 zimezingirwa na maji na nyingine 1,143 zimebomoka kutokana na mafuriko hayo.
 
Waziri Mkuu amewaomba Watanzania wote kutambua tatizo kubwa lililoikabili Taifa na kuwasihi wajitokeze zaidi kuwachangia wenzao wa Kilosa kwa misaada mbalimbali ya mavazi, chakula, madawa na mahema au kitu kingine watakachojaliwa.
 
Amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Issa Machibya kumfukuza kazi mara moja mtumishi yeyote atakayebainika anatumia misaada ya wahanga kwa maslahi yake binafsi. “Ninawasishi viongozi wa Halmashauri simamieni vizuri zoezi la kugawa misaada hii ili kuwe na mgao wa haki kwa watu wote... atakayebainika anafanya kinyume, RC mfukuze kazi mara moja kwa sababu huyo hafai kuwa kiongozi.“
 
“Haiwezekani watu hapa wana shida, wenzio wamejinyima na kuwachangia hao wenye shida halafu anakuja kiongozi anaamua kutumia misaada kwa maslahi yake... nasikia wengine wanauza. Huyo hatufai, RC ukimsikia fukuza mara moja,“ alisema huku akishangiliwa na wakazi wa Kilosa Town.
 
Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam leo jioni (Jumamosi, Januari 9, 2010). 
                               
(mwisho)
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd