Home | News | Tumechagua maendeleo lakini tunaiua sayari yetu - Pinda
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwa na marais, Mwai Kibaki wa Kenya (wapili kushoto) na Yoweri Museveni wa Uganda ktika sherhe za kuapisha baraza jipya la mawaziri la Kenya kwenye viwanja vya ikulu ya Nairobi April 17,2008. Wengine ni Makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musokya (watatu kulia) na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Tumechagua maendeleo lakini tunaiua sayari yetu - Pinda

Vienna,7 December 2009

 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema uharibifu wa mazingira unaoendelea hivi sasa unasababishwa na kazi za uzalishaji zinazotokana na maendeleo ya viwanda duniani kote.
 
Amesisitiza kwamba mbali na maendeleo ya viwanda yanayopigiwa kelele kila mahali bado kuna haja ya kuhakikisha kwamba maendeleo hayo yanazingatia teknolojia zinazotunza mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa 13 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) ulioanza leo (Jumatatu, Desemba 7, 2009) mjini Vienna, Austria.
 
“Leo hii tunashuhudia uharibifu wa mazingira wa hali ya juu... sayari yetu inateketea kwa sababu tumechagua njia ya kuleta maendeleo na hii ni kwa sababu maendeleo ya viwanda vyetu yamezingatia zaidi upatikanaji wa faida kuliko kujali utunzaji wa mazingira,” alisema.
 
Amesema uamuzi wa kutunza mazingira unahitaji utashi wa makusudi wa kisiasa na wa kitaalamu kwa vile wataalamu wanaamini kwamba matumizi ya teknolojia zinazotunza mazingira yanaweza kusaidia kuhifadhi mazingira na wakati huohuo yana maslahi ya kibiashara.
 
Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea hivi sasa yataziathiri zaidi nchi zinazoendelea kuliko nchi tajiri kwa sababu nchi hizo hazina mbinu za kisasa za kuhimili mabadiliko hayo na matokeo yake ni kuandamwa kila mara na ukame wa muda mrefu, mafuriko na vimbunga.
 
Akizungumzia kuhusu juhudi ambazo Serikali imechukua kukabiliana na upotevu wa nishati kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira, Waziri Mkuu alisema Tanzania imetunga sera na mikakati inayolenga kuhakikisha kuna njia endelevu za utunzaji wa mazingira na kubainisha hatua kadhaa ambazo Serikali imechukua hadi sasa.
 
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kutumia nishati ya gesi asilia kwa shughuli za uzalishaji badala ya kuendelea kutumia kuni, mafuta au makaa ya mawe. “Pia tunahimiza matumizi ya nishati kutokana na takataka kama vile mabaki ya miwa, katani na mbao,” alisema.
 
Alisema nishati inayozalishwa na miwa inatoa megawati 38, mabaki ya mbao yanazalisha megawati 18.5 na katani inatoa kilowati 300,” alisema. Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia takataka za katani baada ya kusindika, ulianza Juni 2008.
 
Kuhusu nishati mbadala, Waziri Mkuu alisema Tanzania imetenga maeneo ya mashamba makubwa kwa ajili ya kulima mazao yanayotoa nishati ili kuhakikisha kuna uzalishaji wa uhakika wa mazao hayo.
 
Mawaziri Wakuu waliohutubia leo asubuhi ni Waziri Mkuu wa Kenya, Bw. Raila Odinga na Waziri Mkuu wa Lesotho, Bw. Pakalitha Mosisili ambao walisisitiza haja ya nchi tajiri kuzisadia nchi zinazoendelea ili ziweze kuzalisha nishati kwa kutumia teknolojia zinazohifadhi mazingira. Mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 173 unaendelea kesho na utafungwa Ijumaa jioni Desemba 11, 2009.
 
 (mwisho)
 
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd