Home | News | Waziri Mkuu ahudhuria ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mawasiliano
News
Speeches

Opening remarks by Rt. Hon. Mizengo P. Pinda (MP), The Prime Minister of the United Republic of Tanzania on the African Green Revolution Forum – Accra, Ghana, 2nd September, 2010...

Hotuba ya Shukrani kwa Wabunge kabla ya Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuvunjwa na Mheshimiwa Rais, Ukumbi wa Bunge, Dodoma, 15 Julai 2010...

More Speeches
Recently Documents

kk Quotes

kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.

Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
More Quotes
Videos
Photo Gallery

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akisalimia wakazi katika mpaka kati ya Sumbawanga na Nkasi mkoani Rukwa jana
More Photos
Documents and Publications


mgPrint friendly version mg Email this page

Waziri Mkuu ahudhuria ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mawasiliano

Geneva,5 October 2009

 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amehudhuria ufunguzi rasmi wa  mkutano mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Kimataifa (International Telecommunication Union – ITU) mjini Geneva ambako ameenda kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete.
 
Baada ya ufunguzi huo,  leo asubuhi (Jumatatu, Oktoba 5, 2009) kulikuwa na kikao cha wakuu wa nchi mbalimbali wanaohudhuria mkutano huo.
 
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, kesho (Jumanne Okt. 6, 2009), Mhe. Pinda anatarajiwa kuhudhuria kikao cha pamoja cha Wakuu wa Nchi na wakuu wa mashirika na makampuni  mbalimbali ya kimataifa yanayoshughulikia masuala ya mawasiliano.
  
Mkutano huo utajadili wajibu mkubwa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendeleza uchumi. Katika mkutano huo kutakuwa na kikao maalum  cha wakuu wa nchi.
 
Serikali inatilia mkazo uendelezaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi.
 
(mwisho)
 
Help | Disclaimer | Privacy | Site Feedback
Copyrights ©2008-2010, The United Republic of Tanzania, Prime Minister All Rights Reserved
Designed and published by DataVision International (T) Ltd