Home News Waziri Mkuu akabidhiwa ripoti ya Kituo cha Mabasi Ubungo
News
mgPrint friendly version mg Email this page

Waziri Mkuu akabidhiwa ripoti ya Kituo cha Mabasi Ubungo

Dodoma,28 July 2009

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea Taarifa kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG),Ludovic Utoh kuhusu mapato na makusanyo ya kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es salaam, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Julai 28, 2009. Mheshimiwa Pinda alimuagiza CAG kufanya uchunguzi huo baada ya kutembelea kituo hicho na kupata malalamiko kutoka kwa wadau Machi mwaka huu.

Click to Enlarge

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekabidhiwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu tuhuma za ukusanyaji wa ovyo na ubadhirifu wa mapato ya Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utouh, alikabidhi ripoti hiyo kwa Mhe. Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu majengo ya Bunge mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Julai 28, 2009).
 
Akikabidhi ripoti hiyo, Bw. Utouh alisema Ofisi yake inakamilisha pia ripoti nyingine ya uchunguzi aliouagiza Waziri Mkuu kuhusu makusanyo ya mapato ya Soko Kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
 
“Hiyo ya Kariakoo tunaikamilisha, na itakuwa tayari kukabidhiwa ifikapo Agosti 15 au kabla ya hapo,” alisema Bw. Utouh.
 
Waziri Mkuu aliagiza ufanywe uchunguzi (Perfomance Audit) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu mapato na matumizi ya makusanyo ya Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko la Kariakoo ili kuboresha mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Mhe. Pinda alitoa maagizo hayo alipokuwa  akiwahutubia viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake ya siku nne ya mkoa huo Machi 15, 2009 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
 
Katika ziara yake hiyo ya kukagua usafi na mazingira ya Jiji, Waziri Mkuu alibaini pamoja na mambo mengine, Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko Kuu la Kariakoo ni maeneo mawili ambayo yangeingiza mapato makubwa kwa Jiji lakini ukusanyaji wake ni wa hovyo na kuna tuhuma za ubadhirifu.    
                                      
 (mwisho)
mgPrint friendly version mg Email this page
Speeches

Remarks by Honourable Mizengo P. Pinda (MP), Prime Minister of The United Republic of Tanzania, during the First Annual Art Camp at Kilimanjaro Hotel Kempinski, 05 February 2010.
Speech by Honourable Mizengo P. Pinda (MP), Prime Minister of The United Republic of Tanzania, at the official opening of the Second East and Central African Social Security Association (ECASSA) Policy Makers’ Workshop on 29th January 2010, at Nyumbani Hotels & Resort In Mwanza
More Speeches
kk Quotes

“Mvaa kiatu ndiye anayejua wapi kinambana. Sisi ndiyo tunaovaa kiatu cha kuendeleza nchi hii … tunajua wapi bado na wapi tayari. Kila mmoja kwa eneo lake aseme wapi bado na nini kifanyike na kifanyike vipi, semeni kwa ufasaha tukosoane tujenge nchi yetu…”

Ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa TPSF, 
Kunduchi Beach, Dar es Salaam,  
16 Machi, 2009

More Quotes
Videos
Photo Gallery
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Hasan Wilayuda baada ya mazungumzo yao rasmi jijini Jakarta Septemba 10, 2009. Mheshimiwa Pinda yuko nchini Indonesia kwa ziara ya kikazi.
More Photos
Documents and Publications