Logo
Saturday, 10 February 2018 00:00    PDF 

Waziri Mkuu amjulia hali Mwenyekiti wa CWT Singida

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) mkoa wa Singida, Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Akiwa hospitalini hapo leo (Jumamosi, Februari 10, 2018), Waziri Mkuu amesema amefarijika baada ya kumkuta Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa vizuri.

Pia Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti pacha walioungana, Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikisha afya zao zinaimarika na wanarejea katika shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wake, Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

Kwa upande wao, Maria na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za matibabu wanazozipata na kwa sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kuwajulia hali na kumtakia heri katika shughuli zake

-ends-

 

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday50
mod_vvisit_counterYesterday107
mod_vvisit_counterThis week50
mod_vvisit_counterLast week753
mod_vvisit_counterThis month2960
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days525145
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved