Logo
Friday, 07 July 2017 00:00    PDF 

Aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri aagwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, Bw. Hassan Shebuge.

Marehemu Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7, 2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017) katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

Bw. Shebuge alifariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali. Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi.

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”

Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.

Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.

-ends-

 

 
Our website is...
 
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday50
mod_vvisit_counterYesterday107
mod_vvisit_counterThis week50
mod_vvisit_counterLast week753
mod_vvisit_counterThis month2960
mod_vvisit_counterLast month3555
mod_vvisit_counterAll days525145
Copyrights ©2013, The United Republic of Tanzania, Prime Minister's office All Rights Reserved